The House of Favourite Newspapers

Je, Tunafuata Kauli ya Rais ya ‘Kufyatua Tu’ au Uzazi wa Mpango? – Video

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile amesema Serikali haijaweka ukomo wa idadi ya watoto ambao mtu anatakiwa kuzaa bali kila mmoja azae kulingana na uwezo wake wa kuwatunza.

 

Dkt Ndungulile ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Novemba 7, 2018 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalumu CHADEMA, Susan Lyimo na kusema kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa mwezi uliyopita mkoani Simiyu ya kuwataka wananchi waendelee kuzaa idadi ya watoto wanaowataka haijakinzana na sera ya uzazi wa mpango hivyo Rais alikuwa sawa kusema “fyatueni tu!”.

VIDEO: MSIKIE HAPA AKIFUNGUKA

Comments are closed.