The House of Favourite Newspapers

Je, Tunahitaji Uzoefu wa Kazi Ili Kuweza Kuajiriwa?

0

IMEKUWA ikiwapa wakati mgumu sana hasa wale wanaokuwa wamemaliza masomo yao kwa muda mfupi na kuingia katika harakati za kutafuta ajira. Ofisi nyingi sana hasa Mashirika Binafsi (yasiyo ya Kiserikali) na Makampuni binafsi yamekuwa yakiongeza suala la Uzoefu wa kazi kama kigezo cha kupata ajira. Hivyo kampuni ya simu ya Infinix ikaona nivyema kuwakutanisha vijana kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa vyuo kuweza kujadili suala hili kupitia mdahalo unaosema “Je, tunahitaji uzoefu wa kazi ili kuweza kuajiriwa?” ambapo ulifanyika katika Ukumbi wa Sahara Ventures uliopo Morocco siku ya Jumamosi Tarehe 10/04/2021.

Mdahalo huu uliwataka vijana kujigawa katika vikundi viwili wenye kukubaliana na mada ambao walifahamika kama Kundi Black na kundi White wenye kupinga kwamba ili kuajiriwa uzoefu si kitu cha lazima. Mdahalo huu uliongozwa na watu maarufukama vile MC. Anthony Luvanda, Bi. Shamila Mshangama na Mr. Erick Benard (Mr. Ben)

Mchuano ulikuwa ni mkali mno kuanzia kwenye vikundi hivyo viwili hadi kwa wageni waalikwa ambao ndio walikuwa kama majaji na waongozaji wa mdahalomzima.

Bi. Shamila alianza kwa kuipinga mada  “kupata kazi sio lazima uwe umeajiriwa maana unaweza kujiajiri kwakuwa na taasisi ambapo unaweza kuonwa kutokana na juhudi ulizofanya, hivyo utakuwa umepata uzoefu kupitia hapo lakini hujaajiriwa”.

Lakini pia MC Luvanda aliikataa hoja kwa kusema “unaweza kuwa huna uzoefu wowote na bado ukafanya vizuri saana na mwenye uzoefu asifanye vizuri pia”.

Vijana wote katika makundi yao nao walionekana kuwa wamejiandaa vyakutosha kila upande ulikuwa na hoja zenye kujitosheleza iliyopelekea kutopata mshindi mmoja kwani kila mmoja aliibuka kidedea na kuondoka na zawadi mbalimbali kama vile Simu, Tshirt, Wireless Keyboards za kompyuta pamoja na Note 8 package iliyokuwa na vitu mbalimbali kama (Mwamvuli, Notebook, Power bank, chupa ya chai/maji, zilizoandaliwa na Mdhamini Mkuu ambayo ni kampuni yenye kujihusisha na uzalishaji wa simu janja Infinix Mobile.

Infinix Pamoja ya kuwa ni kampuni iliyojikita kwenye soko la simu lakini pia ni kampuni yenye kumjali zaidi mwanafunzi wa leo kwa kumuandaa kwajili ya kesho yake. Kupitia XTOK Infinix imeweza kuwafikia wanafunzi wengi sana kwa wakati mmoja ambapo kila mwanafunzi hujifunza kitu kipya katika Tafrija hii ya XTOK.

Infinix mobile Tz kuwaahidi vijana na wote waliohudhuria kwenye mdahalo huu kuwa watakuwa nao pamoja kwenye shughuli zote za vijana na pia kuwasihi wasikose mdahalo ujao kwakuwapa nafasi pia wao kuchagua mada ambayo itakuwa ya Xtok inayofata, mada inaendelea kwenye kurasa zao za kijamii kama Facebook, Instagram na Twitter na pia kwenye kiunga chao cha Xclub.

Tembelea link hii kuona mdahalo huu ulivyoenda. https://www.instagram.com/p/CNmyuLYHfO/?igshid=o67ietlqew7k

Leave A Reply