The House of Favourite Newspapers

Je, una kipaji cha kuchekesha? Global TV imetangaza fursa

KAMA unajijua unacho kipaji cha kuchekesha na kuwavunja watu mbavu, basi hii inaweza kuwa habari njema sana kwako.

 

Kituo bora cha runinga mtandaoni cha Global TV Online, kimetangaza fursa adhimu kwa vijana wenye vipaji vya kuchekesha ambapo litafanyika shindano maalum na watakaoibuka washindi, watapata shavu la nguvu la kusaini mkataba wa kufanya kazi na Global TV.

 

Kitakachofanyika, ni kwamba vijana wenye vipaji, watashindanishwa vikali kumtafuta bingwa wa kuchekesha. Pengine umeshaanza kupatwa na mzuka na unajiuliza utashiriki vipi? Jibu ni rahisi sana, kama unaamini unacho kipaji kikubwa, jirekodi kipande kifupi ukichekesha kwa kutumia simu yako, kisha tuma ‘clip’ yako unayoamini kwamba ni kali kuliko zote, kupitia email ya [email protected] kisha kaa ukisubiri majibu wakati jopo la wataalamu wa sanaa, wakivichambua vichekesho hivyo kumpata mkali kuliko wote.

 

Mshindi atakayepatikana, atasainishwa mkataba na kuungana na timu ya nguvu ya Global TV inayohusisha watangazaji, wapigapicha, ‘video editors’ na wengine kibao wanaofanya kazi kubwa kuhakikisha Global TV Online inaendelea kuwa namba moja.

 

Pia kwa wewe unayependa kufuatilia habari mbalimbali, kama matukio makubwa yanayotokea nchini, habari za wanasiasa, wanamuziki na mastaa mbalimbali, basi Global TV inakata kiu yako kwani imesheheni kila unachokihitaji.

 

Namna ya kujiunga, ni rahisi sana! Fungua youtube kwa kutumia simu yako, laptop au kompyuta kisha andika Global TV Online, ikifunguka bofya kwenye maneno yaliyopo kwenye alama nyekundu yaliyoandikwa SUBSCRIBE, malizia kwa kubofya alama ya kengele ambapo sasa utakuwa na uwezo wa kuona habari zote mpya zinazorushwa kupitia Global TV.

 Stori: Mwandishi Wetu

Comments are closed.