The House of Favourite Newspapers

Jean Baleke Aitamani Yanga Awaita Mashabiki wa Simba Uwanja wa Mkapa

0
Jean Baleke (kulia) akifanya yake.

STRAIKA tishio wa Simba raia wa DR Congo, Jean Baleke, amesema yuko tayari kufia uwanjani ili ahakikishe anaifunga Yanga na kuipatia ushindi wa heshima timu yake, hivyo Wanasimba wanatakiwa kujua kuwa, Jumapili ni siku ya kwenda kufurahi.

Baleke amejiunga na Simba kwenye dirisha dogo la usajili msimu huu, ambapo tayari amefunga mabao 7 katika Ligi Kuu Bara, akimkimbiza kinara Fiston Mayele mwenye mabao 16.

Jumapili ya wiki hii, Simba inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar. Mchezo wa mzunguko wa kwanza, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally, alisema amezungumza na Baleke kuhusu mchezo huo na kusema kwamba anahamu kubwa ya kuwafunga Yanga ili kuwafurahisha mashabiki na wanachama wa Simba.

“Baleke yupo tayari kuwafunga Yanga, maana alisema huo ndio mchezo wake wa kwanza mkubwa hapa nchini, hivyo amejipanga kuhakikisha anapata matokeo ya kuwapa ushindi na furaha Simba,” alisema Ahmed.

STORI NA MUSA MATEJA

MBUNGE AANGUA KILIO BUNGENI, AWAACHA WABUNGE HOI – “TEMBO WANAUA WANANCHI WETU”

Leave A Reply