Jela Miaka 45 kwa Kumbaka na Kumpora Mwanamke Mjerumani

MAHAKAMA ya Wilaya ya Iringa mkoani Iringa imemuhukumu Selemani Juma mwenye umri wa miaka 36 kwenda jela miaka 45 na fidia ya Tsh milioni moja baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanamke raia wa Ujerumani na kupora simu na pesa taslimu Tsh laki moja.

Kwa upande mwingine, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi akitoa taarifa ya matukio ya uhalifu, amesema kijana huyo baada ya kutenda kosa hilo alitokomea kusikojulikana lakini kwa kiasi kikubwa wananchi wakashiriki kutoa taarifa mpaka akakamatwa kwake.


Toa comment