The House of Favourite Newspapers
gunners X

Jeneza la Simba, Yanga Lilivyozua Gumzo Taifa

MASHABIKI wa Simba jana waliendelea na mbwembwe zao kwenye mechi dhidi ya Yanga baada ya kuingia na jeneza lenye bendera za watani zao hao ambao nao walijibu mapigo.

Simba na Yanga zilipepetana jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ukiwa ni mchezo wa kwanza kwao msimu huu.

 

Championi Jumatatu ambalo lilikuwepo uwanjani hapo, liliwashuhudia mashabiki hao wa Simba wakiwa ndani ya uzi mweupe na mwekundu wakiwa na jeneza hilo huku wakishangiliwa na wenzao.

 

Lakini baadaye kidogo, Yanga nao walijibu mapigo baada ya mashabiki wao kuingia na jeneza lililovalishwa bendera zenye rangi nyekundu na nyeupe ambazo hutumiwa na Simba.

Siyo mara ya kwanza kwa timu hizi mashabiki wake kufanya vituko uwanjani.

 

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Comments are closed.