The House of Favourite Newspapers

TANGA: WAHAMIAJI HARAMU 28 WAKAMATWA MSITUNI

WAHAMIAJI haramu wapatao  28 ambao ni raia wa Ethiopia wamekamatwa kwenye Msitu wa Maili Kumi uliopo wilayani Handeni mkoani Tanga baada kutelekezwa huku wakionekana kuchoka kwa kukaa muda mrefu bila kula.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ambae pia ndiye Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe,  ametoa onyo kwa wale wanaojihusisha na biashara hiyo na kusema kuwa serikali itapambana nao.

 

Aidha, mkuu huyo wa wilaya amedai kuwa wanafanya utaratibu wa kuwasafirisha hadi jijini Tanga ili mamlaka husika ziweze kuchukua hatua zaidi.

Picha ya Maktaba.

Comments are closed.