The House of Favourite Newspapers

Jengo Refu Lalipuka na Kuporomoka Irani, Wengi Wauawa

jengo-maafa-1

TEHRAN: JENGO kubwa limelipuka moto na kuporormoka hivyo kusababisha maafa makubwa katika Mji Mkuu wa Iran, Tehran mapema leo Alhamisi, Januari 19, 2017.

jengo-maafa-2

Jengo hilo likiwaka moto.

Ripoti zinasema kuwa, wazima moto 200 walikabiliana na moto huo kwenye jengo hilo la ghorofa 17 kwa saa kadha, kabla ya kuporomoka chini kwa sekunde chache ambapo imeelezwa kuwa wazima moto wengi wanahofiwa kuaga dunia na watu 200 kujeruhiwa kwenye mkasa huo.

jengo-maafa-3

Majeruhi wakiokolewa.

Jengo hilo ambalo ujenzi wake ulikamilika mwaka 1962, lilikuwa wakati mmoja jengo refu zaidi mjini Tehran ambapo moto huo unaripotiwa kuanza majira ya saa 04:30 GMT.

jengo-maafa-4Magari kumi ya kuzima moto yalifika eneo hilo na vituo vya runinga viliripoti kuwa wazima moto kadha walikuwa ndani ya jengo wakati liliporomoka.

jengo-maafa-5

Vilio vikitanda eneo la tukio.

Kituo kimoja cha runinga cha serikali kilinukuu afisa mmoja akisema kuwa kati ya watu 50 na 100 wanasadikiwa kukwama chini ya vifusi na haijulikani kama ni wazima ama wameaga dunia tayari.

Comments are closed.