The House of Favourite Newspapers

Jennifer Lopez Alinizingua- Shilole

0

Msanii Shilole amefunguka na kutoa sababu zilizopelekea yeye kushindwa kufanya ngoma na msanii Jennifer Lynn Lopez, alimaarufu kama JLo na kusema aliona anamzingua hivyo ikabidi aachane naye.

Shilole alisema hayo alipokuwa kwenye interview na EATV na kudai kweli alionana na meneja wa msanii huyo na kuongea naye lakini baadaye ilishindikana kwa sababu yeye Shilole alishindwa kurudi tena Marekani kutokana na mambo yake kuwa mengi.

“Aisee ilishindikana maana mimi sikupata muda tena wa kwenda Marekani kwani kuna mambo yangu nilikuwa nafanya hapa nyumbani ya kimuziki na familia, hivyo muda ukawa unanipita hivi na ukiangalia Jennifer mwenyewe naye ndiyo kwanza alikuwa katoa ule wimbo  ‘Ain’t Your Mama’ nikaona tusisumbuane sana mwache tu aendelee na mambo yake mimi nitamtafuta Nick Minaj popote alipo” alisema Shilole 

Leave A Reply