The House of Favourite Newspapers

JESCAR NGAISE: KINDA WA KIKAPU MWENYE UCHU WA KUVAA VIATU VYA JOKATE

Mwanafunzi wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Brothers, Jescar Ngaise.

 

“NDOTO zangu kubwa nilizonazo ni kuwa kiongozi kwenye hii nchi kama ilivyo kwa Jokate Mwegelo, ambaye ni balozi wa mpira wa kikapu nchini lakini pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe. “Maarifa aliyonayo, jitihada, hekima, kujituma, kujiamini na mambo mengi, ndiyo silaha iliyomfi kisha hapo alipo, lakini bado nina matumaini juu yake kuwa atafi ka mbali kitu ambacho kinanisukuma kuendeleza mapambano kwenye elimu na hata michezo ili niwe kama yeye na zaidi.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.

 

 

 

“Kwa sasa mimi bado ni mwanafunzi wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Brothers iliyopo maeneo ya Gongo la Mboto, lakini pia ni mchezaji wa kikapu ninayeitumikia timu ya Ukonga Queens hapa jijini Dar.

Jescar Ngaise.

“Nikiwa bado ni binti mwenye umri wa miaka 17, nimeshaanza kupita na kujifunza anayofanya Jokate nikiamini kwamba siku moja Watanzania wataniamini na kusimama imara kunisikiliza kwa manufaa ya taifa zima,” anaanza kueleza Jescar Ngaise.

 

Ngaise anayevalia jezi namba 10 uwanjani, alianza kujikita rasmi kwenye mafunzo ya mpira wa kikapu mwaka 2014 akiwa bado ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Juhudi iliyopo jijini Dar.

Anasema kuwa, kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo katika mchezo huo, ilichukua muda mfupi kuzifahamu sheria zake na namna ya kucheza hadi hapo uongozi wa Ukonga Queens ulipofanya naye mazungumzo na kumsajili kuwa mchezaji wao halali.

 

Baada ya Ukonga Queens kumsajili, Ngaise alifanikiwa kupata namba na kuitumikia vema timu hiyo dhidi ya wapinzani kupitia mashindano tofauti. Miongoni mwa mashindano ambayo Ngaise ameshiriki hadi sasa ni Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA) ambayo kwa msimu huu inatarajiwa kuunguruma mwezi ujao.

 

Mashindano mengine ambayo amewahi kupata namba ni yale ya Taifa ambayo pia mwaka huu yalimalizika kule mkoani Simiyu.

KWA NINI JOKATE?

“Kwanza kabisa ni mwanamke anayejitambua na kujua nini anafanya, ana upendo kwa watu wote, anapenda vijana wasome na wajikite kwenye michezo jambo ambalo ni zuri na lenye manufaa kwetu, ukizingatia kwamba bila elimu huwezi kufi ka popote na kama utafi ka basi jamii haitakuamini sana.

 

“Niwe mkweli, mimi namkubali sasa Jokate na ninatamani siku moja nije kuvaa viatu vyake, nisimame na kuongea na Watanzania kuhusu mambo mengi ya kimaendeleo. “Jambo lingine alilonifurahisha Jokate ni ile programu yake
aliyoianzisha ya ‘Tokomeza Zi ro’, kwa hili nampongeza sana, nataka ajue tu vijana wake tupo nyuma tunamuangalia kwa jicho la tatu tukitamani na sisi siku moja tuvae viatu vyake,” anaeleza.

BONGO HADI AFRIKA KUSINI

I Mwaka 2017, Ngaise alipata bahati ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuwakilisha nchi kwenye mafunzo ya mpira wa kikapu yajulikanayo kama ‘Basketball Without Bodder’ kule nchini Afrika Kusini. Hapa anaelezea namna alivyoipata nafasi hiyo: “Bahati hiyo niliipata baada ya kuiwezesha timu yangu ya Tanzania kushika nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Kenya mwaka huo wa 2017. “Nikiwa kwenye mafunzo, nilijifunza vitu vingi kuhusiana na mpira wa kikapu lakini pia, nimeongeza idadi ya marafi ki wa mataifa mbalimbali ambao tulikutana na kubadilishana mawazo.”

 

WAZAZI WALITAKA KUMZUIA

Ngaise ambaye ni nahodha wa timu ya taifa na ile ya Ukonga Queens, anaendelea kusema kuwa: “Kwanza kabisa nilianza kucheza kikapu kama masihara nikiwa shule, lakini timu yangu ya Ukonga ilipotaka kunisajili nilifi kisha taarifa nyumbani.

 

“Wazazi walipokea suala hilo kwa mikono miwili lakini balaa lilianza kujitokeza pale nilipokuwa nachelewa kurudi nyumbani kutokana na mazoezi ya jioni pamoja na foleni za barabarani, wakataka kunizuia kuendelea kucheza mchezo huo. “Mimi ni mtoto wa kike na siku zote wazazi wanatuchunga sana ili mabinti zao tusipite njia hatarishi, kwa kuwa nilikuwa napenda kikapu, nilikaa na wazazi wangu chini na kuzungumza nao kwa kina hadi wakanielewa.”

KUELEKEA RBA

Mwandada huyo anaelezea jinsi alivyojipanga na Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar (RBA) inayotarajiwa kuanza mwezi ujao kwa kusema: “Amsha amsha ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa (RBA) ndiyo zinaendelea, timu mbalimbali zimeanza kujifua kila moja kujihakikishia ubingwa, lakini mimi naahidi msimu huu Ukonga Queens tutakuwa mabingwa.”

MAKALA NA SHARIFA MMASI | CHAMPIONI JUMAMOSI

Comments are closed.