The House of Favourite Newspapers

KIM NANA APATA KIGUGUMIZI ‘KUBANJUKA’ NA MTANGAZAJI

Lilian Kessy ‘Kim Nana’

MUUZA nyago maarufu Bongo, Lilian Kessy ‘Kim Nana’ ambaye amewahi kutajwa kulionja penzi la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amepata kigugumizi baada ya kubanwa juu ya kubanjuka kimapenzi na mtangazaji wa East Africa Television, Tbway.

Awali, chanzo makini kililieleza Risasi Jumamosi kuwa, Kim Nana kwa sasa yupo kwenye penzi jipya na mtangazaji huyo ambapo siku ya Valentine mwanadada huyo alimnunulia Tbway saa na mwanaume huyo alimpa viatu.

Baada ya kupata ubuyu huo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Kim Nana ambapo alipata kigugumizi kwenye kujibu ambapo ilikuwa hivi;

Risasi: Kim kuna habari kuwa unatoka kimapenzi na mtangazaji Tbway, hili likoje?

Kim Nana: Kwa nini umeniuliza huyo?

Risasi: Kwa sababu habari zinaeleza ndiye mpenzi wako kwa sasa na siku ya Valentine mmenunuliana zawadi, vile viatu ulivyoposti Instagram alikununulia yeye.

Kim Nana: Mmhh! Vile viatu nimenunuliwa na mpenzi wangu siku ya Valentine ndiyo.

Risasi: Mpenzi wako Tbway?

Kimnana: Aaah jamani eeeh! (akakata simu).

Stori: Shamuma Awadh, Dar

Comments are closed.