The House of Favourite Newspapers

Kemikali nyingine za milipuko zagunduliwa bandari ya Beirut

0

JESHI la Lebanon limesema limegundua tani zaidi ya nne za madini ya kemikali ya ammonia nitrate karibu na lango la bandari ya Beirut sehemu ambapo ulitokea mlipuko mkubwa mwezi uliopita uliosababishwa na mlundiko wa kemikali kama hizo zenye nguvu kubwa ya kulipuka.

 

Kwa mujibu wa tamko la jeshi lililoripotiwa na shirika la habari la serikali (NNA) wahandisi wa jeshi la Lebanon wanalishughulikia jambo hilo.

 

Wakati huohuo wanaofanya juhudi za uokozi wamesema wamepata ishara ya kuwepo watu chini ya vifusi vya majengo yaliyoanguka, na hivyo kuleta matumaini huenda wapo watu walionusurika hata baada ya mwezi mmoja tangu kutokea mlipuko mkubwa kwenye bandari ya mji wa Beirut.

 

Taarifa hiyo imetolewa na maafisa pamoja na vyombo vya habari mjini humo.

Leave A Reply