The House of Favourite Newspapers

Jeshi la Polisi Latoa Elimu ya Uzalendo Kwa Maelfu ya Waumini Kanisa la Ngome ya Yesu

0
Waumini wakimsikiliza kiumakini Afande ASP Dr. Ezekiel Kyogo akilipokuwa akiwapa elimu.

 

 

6 Novemba 2022: JESHI polisi nchini leo limetoa elimu ya uzalendo mbele ya maelfu ya waumini waliofurika kwenye Kanisa la Ngome ya Yesu linaloongozwa na Kuhani Musa Richard Mwacha liliopo Kimara Temboni jijini Dar.

Msafara wa kuingia kanisani ulivyokuwa, Afande ASP Dr. Ezekiel Kygo kulia, kushoto Afande ni ASP Dotto aliyeambatana na Kyogo na katikati mwenye joho lenye msalaba ni Kuhani Musa Richard Mwacha wakiwa kwenye msafara huo.

 

 

Akitoa elimu hiyo kanisani hapo, Mrakibu wa Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ASP) Dr. Ezekiel Kyogo kwa niaba ya mkuu wa jeshi hilo, IGP Camillius Wambura amewataka waumini hao kudumisha ulinzi kuanzia ngazi ya familia kwa kuimarisha malezi bora.

Afande ASP Dr. Ezekiel Kyogo (kushoto) akiendelea kutoa elimu na wasaidizi wake kwenye ibada hiyo.

 

 

Afande Kyogo alisema hayo huku akinukuu vifungu kadhaa vya biblia vinavyoonesha kuwa umuhimu wa suala la ulinzi na usalama tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

 

 

Hivyo basi amewataka waumini hao wasifumbie macho wanapoona viashiria vya matendo ya uhalifu kama vile unapoona mtu anananyemelea kumkwapulia mwenzake nawe kukaa kimya kwakuwa huibiwi wewe amesema hiyo si sawa na haimpendezi hata Mungu.

Msafara wa kuingia kanisani.

 

 

Afande Kyogo alimalizia kwa kuwaambia waumini hao kuwa endapo wakiweza kutengeneza malezi bora kuanzia ngazi ya familia basi tutaangamiza kabisa kizazi uhalifu na kutomeza matukio kama haya panya road, waporaji kwenye bodaboda ‘vishandu’, wezi wa karamu maofisini, wala rushwa na wengineo.

 

 

Katika kuonesha kulipokea vyema somo hilo waumini hao walikuwa wakilipuka kwa mayowe ya shangwe na nderemo kila walipoguswa au  ‘nondo’ ilipowaingia kisawasawa.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY /GPL 

Leave A Reply