Jeshi la Polisi Limesema Tayari Limeanza Kuufanyia Kazi Ushauri wa M/Mwenyekiti wa CCM, Kanali Mtaafu Kinana
JESHI la Polisi limesema limeupokea ushauri wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana wa kupunguza idadi ya Askari wa Usalama Barabarani (Trafiki).
Jeshi la Polisi limesema tayari limeanza kuufanyia kazi ushauri huo.