The House of Favourite Newspapers

Mahakama Yakubali Halima Mdee na Wenzake 18 Kuhojiwa

0
Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam imewataka  Halima Mdee na Wenzake saba kufika mahakamani hapo Agosti 26 Agosti 2022 , kwa ajili ya kuhojiwa na Mawakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhusiana na  viapo vyao.
Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa Chadema, Peter Kibatala leo Julai 29, 2022kuwasilisha maombi mahakamani hapo Kuu kuwapatia wito wa kuwaita mahakamani hapo wabunge hao wa viti maalumu pindi kesi yao itakapoanza kusikilizwa ili waweze kuwahoji mbele ya Jaji Cyprian Mkeha.
Akiwasilisha maombi Hayo Kibatala amedai siku ya usikilizwaji wanakusudia Kuwaita Halima Mdee, Nusrat Hanje, Grace Tendega, Ester Matiko, Ester Bulaya, Cecilia , na  Mwaifunga ma Jesca Kishoa kwa ajili ya kuwahoji juu ya viapo vyao walivyowasilisha mahakamani hapo
Hata hivyo, mawakili wanaowakilisha kina Mdee wakiongozwa na Aliko Mwamanenge amedai baada ya mawakili wa wajibu maombi kuwasilisha kiapo kinzani na wakiona ipo haja ya kuwaita baadhi ya viongozi wa Chadema mahakamani hapo kwa ajili ya kuwahoji basi watafanya hivyo.
Baada ya maelezo hayo, Jaji Mkeha ameridhia ombi la Chadema la kuwaita wabunge hao ili waweze kufika mahakamani kuhojiwa siku ya usikilizwaji wa kesi.
Aidha amewataka wajibu maombi ambao ni Chadema na, NEC na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwasilisha kiapo kinzani mahakamani hapo Agosti 5 mwaka huu na iwapo wapeleke maombi watakuwa na majibu basi wajibu Agosti 10,2022. Kesi itaanza kusikilizwa Agosti 26,2022
Halima Mdee na wenzake 18 wamefungua kesi mahakamani hapo wakipinga kuvuliwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Leave A Reply