The House of Favourite Newspapers

Jeshi La Polisi Na SGA Security Waahidi Kuendelea Kushirikiana

0
Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Security, Bw. Eric Sambu, akizungumza wakati wa hafla ya kuwaenzi waanzilishi wa kampuni hiyo na kuwaaga wastaafu. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Mtatiro Kitinkwi (mwenye sare wa tatu kulia)

Kampuni ya SGA Security ambayo ni kampuni kongwe na kubwa zaidi ya ulinzi nchini imeahidi kuendeleza utamaduni wake wa mahusiano ya karibu wa kikazi na Jeshi la Polisi Tanzania.

Ahadi hiyo imetolewa mwishoni mwa juma, wakati wa maadhimisho ya kuakumbuka waasisi wa kampuni hiyo Hayati Philemon Mgaya na Hayati Edmond Tongeren wa kutoka nchini Uholanzi.

Marehemu Mgaya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) na Mshirika wake kutoka Uholanzi, marehemu marehemu Tongeren, waliianzisha kampuni hiyo hapa nchini Tanzania mwaka 1984.

Wawili hao wote walifariki dunia mmoja Julai 13 na mwingine Julai 14, ingawa kwa miaka tofauti, ambapo uongozi wa kampuni hiyo ulioko sasa umeamua kufanya kumbukumbu yenye lengo la kuenzi maisha ya waasisi hao ambapo waliahidi kuendeleza maono waliyokuwa nayo viongozi hao waasisi. kusherehekea maisha yao na kuahidi kuendeleza maono waliyokuwa nayo.

Wastaafu wa Kampuni ya SGA Security wakionesha zawadi zao wakati wa hafla ya kuwaaga.

Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Security, Eric Sambu, alisema kuwa kampuni hiyo sasa inaajiri zaidi ya wafanyakazi 5,000, ambapo alisema idadi hiyo imeanza kuongezeka baada ya kushuka hivi karibuni kutokana na ongezeko la ghafla la kima cha chini cha mishahara kulikosababisha baadhi ya wateja kutafuta huduma zingine za bei nafuu.

“Tumepitia mengi lakini kila tunapokumbana na changamoto huwa tunakabiliana nazo na kupata mafanikio makubwa”, alisema Sambu.

Aliongeza kusema kuwa siri ya mafanikio ya kampuni hiyo ni ushirikiano mzuri ulionao uongozi na wadau muhimu katika biashara jambo ambalo alisema ni utendaji mzuri wa kampuni hiyo swala endelevu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Mtatiro Kitinkwi (mwenye sare wa tatu kulia ) picha ya pamoja na wastaafu wa kampuni ya SGA Security wakati wa hafla ya kuwaaga na kuwaenzi waanzilishi wa kampuni hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Eric Sambu.

Akitolea mfano, Bw Sambu alisema ni pamoja na ushirikiano wa karibu na Jeshi la Polisi Tanzania, ambapo alisema ni ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote mbili ambapo alielezea azma ya SGA Security kuuendeleza ushirikiano huo.

Aidha alisema katika hafla hiyo, pia waliwatunukia zawadi mbalimbali watumishi a kampuni hiyo waliofikiwa umri wa kustaafu.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wafanyikazi walioitumikia kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 20, ambapo walipata fursa ya kujiunga na klabu maalum ya kampuni hiyo ijulikanayo kama Club 20, ambayo inahusisha zaidi ya wafanyakazi 200 wa kampuni hiyo ambao tayari washaitumikia kwa miaka 20 na Zaidi maeneo mbalimbali Tanzania inakofanya shughuli zake.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni ACP Mtatiro Kitinkwi, aliupongeza uongozi wa kampuni ya  SGA Security kwa kuwa mshirika wa karibu wa serikali kupitia jeshi la polisi nchini.

Akitoa mfano wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili, ACP Mtatiro alisema ni ushirikiano ambao SGA Security hutoa kupitia doria hususan mwishoni mwa wiki.

“Tumeshuhudia mwitikio wa kuvutia kutoka kwa SGA tunapohitaji msaada wao kwa miaka mingi na hatushangai pale mnapopongezwa kama kampuni bora ya ulinzi kwa upande wa sekta binafsi”, alisema.

Alitoa wito kwa makampuni mengine ya ulinzi kuiga mfano mzuri wa utuendaji bora wa shughuli za ulinzi unaofanywa na kampuni ya SGA Security.

Pia aliipongeza kampuni ya SGA Security kwa kujali maslahi ya wafanyikazi walioajiriwa na kampuni hiyo ikiwemo kuwatunukia wastaafu walioitumikia kampuni hiyo.

“Katika makampuni mengi, hakuna kazi hizo na hata uzingatiaji wa kimsingi wa sheria ni suala. Thamani ya Usalama wa SGA kwa wafanyakazi ni jambo ambalo makampuni yote ya ulinzi yanafaa kuiga”, aliongeza.

Aidha aliwapongeza wale walioajiriwa na kampuni hiyo kwa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu mkubwa jambo ambalo alisema linaijengea heshima kubwa kampuni ya SGA Security.

“Tumesikia matukio mbalimbali yakihusisha baadhi ya waajiriwa wa taasisi zingine za ulinzi jambo ambalo hatujawahi kuyasikia yakihusisha wafanyakazi wa SGA Security, wito wangu kwenu ni kuhakikisha mnailinda sifa hii nzuri”, alisema.

“Pia nichukue fursa hii kuupongeza uongozi wa SGA Security kwa kuzingatia maelekezo yote yanayotolewa na jeshi la polisi yanayohusiana na uajiri pamoja na uendeshaji wa makampuni ya ulinzi ya kibinafsi”, alisema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Kampuni za Ulinzi za Binafsi nchini (TUPSE), Charles Basondole, alitoa shukurani zake kwa uongozi wa SGA Security kwa kujali maslahi ya wafanyakazi, wakiwemo waliostaafu, ambapo alisema haikufanya makosa kuitunuku SGA Security zawadi ya mwajiri kwa mwaka wa 2022-2023 hivi karibuni.

Naye Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya SGA Bw Oscar Mgaya amelishukuru jeshi la polisi kwa ushirikiano wa karibu inaotoa kwa kampuni hiyo.

Alisema waanzilishi wa kampuni hiyo pia walijenga msingi mzuri wa mahusiano kati ya kampuni hiyo na taasisi zingine na ndiyo maana serikali na vyama vya wafanyakazi husiriki shughuli zote zinazofanywa na SGA Security.

Aliendelea kusema kuwa kampuni hiyo imekua ikipata mafanikio katika utoaji huduma zake huku ikizingatia taratibu zote za kisheria zinazohusiana na utoaji huduma hizo.

“Wakati wateja wakiendelea kuwa karibu na huduma zinazotolewa na SGA Security, sisi tunaahidi kuendelea kutengeneza mazingira mazuri ya utoaji huduma zetu:, alisema.

Leave A Reply