Viongozi wa Simba Mwanza Wavuliwa Nyadhifa Zao
MASHABIKI na wanachama wa Klabu ya Simba ya Mkoa wa Mwanza kwa pamoja wameazimia kwa kauli moja kuuvua madaraka uongozi wa matawi ya Simba mkoa wa Mwanza mara baada ya Uongoz huo kushindwa kufuata Katiba na taratibu walizjiwekea. Akiongoza mkutano huo kaimu Mwenyekiti wa muda Salya Ludanha amesema wameamua kuja na maamuzi hayo magumu mara baada ya Uongozi uliokuwa madarakani kwa kipindi cha miaka minne sasa kushindwa kuitisha vikao vya kikanuni ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwaunganisha wanachama wa Simba ambapo walionekana kuzidiwa mipango na wapinzani wao wa jadi Yanga.
Salya amesema kwa sasa Mamlaka ya uratibu wa shughuli za Simba Mwanza utafanyika na viongozi wa mpito waliopitishwa na mktano mkuu wa Mkoa huku wakisubili kutangaza tarehe ya Mkutano Mkuu wa uchaguzi Mwezi wa agosti Mwaka huu. Uongozi uliondolewa madarakani baada ya Mkutano huo kufanyika ni pamoja na ni Aliyekuwa Mwenyekiti wa matawi ya Simba mkoa wa Mwanza Phillemon Tano, Ishuu Ashraf Makamu Mwenyekiti, Philbet Kabago Katibu wa Mkoa, Mohamed Badru Mhasibu Mkoa, Fatma Shemweta Mjumbe Mkoa, Aggrey Gombanila, Mjumbe Mkoa.
baada ya maamuzi hayo kufanyika sasa rasmi Uongozi Mpya wa mpito wa matawi ya Simba mkoa wa Mwanza utaongozwa na Kaimu Mwenyekiti Salya Ludanha, Katibu Tawfyq Massini,pamoja na Mratibu wa Hamasa Mkoa Nassibu Namocha ambapo kwa mujibu wa maamuzi ya mkutano huo viongozi hao ndio wataendelea kuwa viongozi wa Simba Mwanza mpaka pale tarehe ya uchaguzi wa Viongozi wa matawi hayo utakapotajwa mwezi Agost.
Na Oscar Mihayo- GPL