The House of Favourite Newspapers

Jeshi Nchini Myanmar Lawanyonga Wanaharakati Wanne wa Demokrasia

0
mwanaharakati maarufu nchini Myanmar Ko Jimmy

WANAHARAKATI wanne wa Demokrasia wa nchini Myanmar akiwemo mbunge wa zamani wameuawa kwa kunyongwa na Jeshi la nchi hiyo kutokana na kukutwa na hatia ya kujihusisha na njama za kutekeleza matukio ya kigaidi nchini humo.

 

Miongoni mwao alikuwepo mwanaharakati maarufu wa nchi hiyo Ko Jimmy pamoja na mbunge wa zamani Phyo ZeyaThaw ambao kabla ya kunyongwa kwao walihukumiwa kifungo cha maisha jela.

 

Mnamo siku ya Jumatatu familia za marehemu hao zilikusanyika nje ya Gereza la Insein lililopo nchini humo ambalo ni moja kati ya magereza hatari duniani ili kujua hatima za wapendwa wao.

 

Mama mzazi wa Zayar Thaw amesema hakupewa taarifa ni lini mtoto wake atanyongwa hali iliyomfanya ashindwe kuandaa vizuri maziko yake.

Gereza hatari la Insein lililopo nchini Myanmar

Tayari familia zote zimetuma maombi rasmi Serikalini kupewa maelekezo juu ya mauaji ya wapendwa wao.

 

Chombo cha habari cha Taifa hilo Global News kimeripoti kuwa wanaharakati hao wameuawa kwa kunyongwa kutokana na kutoa siri, maelekezo, kupanga njama pamoja na kusababisha kutekeleza mauaji ya kikatili ya raia wasio na hatia.

Mauaji hayo ya kunyonga ni ya mara ya kwanza nchini humo tangu ifanyike hivyo mwaka 1988, hiyo ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Leave A Reply