The House of Favourite Newspapers

Jezi Mpya Simba Kuzinduliwa Mlima Kilimanjaro Ijumaa ijayo – Video

0

UONGOZI wa Simba, umeweka bayana kuwa, jezi mpya za timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao 2023/24 zitazinduliwa Ijumaa ijayo katika Kilele cha Mlima wa Kilimanjaro.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, alisema: “Jezi rasmi za Simba kwa msimu ujao zitazinduliwa Ijumaa ijayo na tutazindua kipekee sana, kwa kuwa tutazindua katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

“Tumefanya hivi kwa kuwa tunataka kuendelea kutangaza utalii wa nchi na kama inavyojulikana Mlima Kilimanjaro ni sehemu ya juu zaidi hapa nchini, tumefanya hivyo kwa kuwa jezi hizi ni kali zaidi.

“Msafara utaondoka hapa Dar Jumatano ijayo na tunawakaribisha wapenzi wa Simba ambao watataka kuungana na sisi kwa ajili ya jambo hili.

“Wakati tunazindua jezi hii huko Moshi, zenyewe zitakuwa zinapatikana maduka yote hapa nchini, jezi za rejareja zitapatikana kwa kiasi cha shilingi 40,000.”

Katika hatua nyingine, Ally aliongeza kwa kusema, Tamasha la Simba Day mwaka huu litafanyika Agosti 6 tofauti na Agosti 8 ambayo imezoeleka.

“Tumelazimika kurudisha siku nyuma kwa kuwa Agosti 10 tutakuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii kule Tanga dhidi ya Singida Fountain Gate FC.

“Kwa hiyo tukifanya Agosti 8, tutawakosesha wachezaji nafasi ya kupumzika, ndiyo maana ikawa siku hiyo.”

MWANDISHI WETU,  SPOTI XTRA

Leave A Reply