The House of Favourite Newspapers

JINI MTU-14

0

“Uchawi maana yake ni mkataba baina ya mchawi na shetani,  wana wa zuoni wanasema, hakuna uchawi unao weza kufanya kazi pasina msaada wa shetani au jini,. hakuna jini yeyote katika ulimwengu huu, anaeweza kumtumikia mwana wa Adamu isipokuwa kwa masharti yaliyo mazito, kama vile, mtu anaweza kuambiwa na Jini, umuandikie maneno ya mwenyezi mungu kwa damu ya hedhi!. Ndugu zangu,. Kwa hakika kuna uhai baada ya kifo, Msiamini kila roho zinazo wajieni kwa hisia, zijaribu roho hizo na mjiulize, je zimetokana na mungu kama sivyo, basi ombeni dua Mungu awaepushe nayo ili msije kuwa miongoni mwa walio kufuru na kuingia katika shimo la moto wa milele, mwenyezi atuepushe na  kadhia hizo Tuseme ishaalah”

“Ishaalah”  Watu wote waliitikia.

Yalikuwa ni maneno ya shekh Othumani Hilal, siku hii ya ijumaa katika moja ya bweni lililofanywa kama musikiti siku ya ijumaa na kanisa siku ya juma pili.

Yalikuwa ni maneno makali mno, maneno yaliyo penya kwa uzuri ndani kabisa ya mtima wangu, yalinitetemesha,  yalitekenya nafsi yangu, kwa kiasi fulani mawaidha yale yalilingana na tabia zangu zilizo kuja bila mwenyewe kutarajia na kujikuta nazipokea kwa mikono miwili.

Ilikuwa yapata  saa saba za mchana, matukio ya jana usiku yakijirudia katika akili yangu kila wakati, sikuwa ni mwenye furaha, kwani nilikuwa nimempoteza mwanamke ambaye ndiye aliyekuwa amebaki katika ulimwengu huu.

Mara nilipata wito  kutoka kwa askari magereza na kutakiwa kuongoza mahala ilipo ofisi ya mkuu wa gereza la bangwe,

Kumekucha tena!.

Nilijua wito ule ni matokeo ya matukio yaliyo tokea usiku wa kuamkia siku hiyo.

Niliingia ndani ya ofisi ile ya mkuu wa gereza na kutakiwa kuketi chini katika viti vilivyo zunguka meza ya duara kulikaliwa na mkuu wa polisi mkoa wa Kigoma{R.P.C}, na {O.C.D}wakati katika kiti cha mbele aliketi mkuu wa gereza la bangwe!.

Nilicheka moyoni huku nikisubiri kuona maamuzi ya hawa binadamu, nilipo keti chini jamaa walinitizama kwa kina huku kila mtu akinitathimini vile alivyo jua yeye,

“Wewe unashida gani na jeshi la polisi.” Hatimae yule R.P.C alihoji.

“Nahitaji kuwa huru wazee..siwatishi ila kama mtaendelea kucheza na mimi..hakika mchezo nauweza” nilijibu kwa kujiamni bila kupindisha maneno wala kumwangalia mtu usoni.

Sikuhitaji kufanya mambo yale yaende kimafumbo mafumbo, nilihitaji waelewe kuwa mimi sikuwa mtu wa kawaida.

“Halafu ukisha kuwa huru?” O.C.D alidakia kwa kiherehere.

“Sinto kuwa na shida na polisi wakuu”

“Na  kama tukikataa je?”

“Mtaona matokeo…nadhani salamu zangu za awali zimekwisha wafikieni.”

“Kwani wewe ni mtu wa aina gani?” Mkuu wa gereza nae aliuliza nyuso zao zikitokwa na jasho ilihali mule ndani kulikuwa na panga boi lililokuwa likizunguka kwa kasi.

“Labda niseme hivi,.mimi ni zaidi ya mtu.. mimi ni zaidi ya mzimu, na mimi ni zaidi ya mwanga,. Eleweni kuwa mnashindana na kiumbe wa ajabu mno, na hakuna dora yoyote itakayo weza kunisimamisha, fanyeni maridhiano upesi vinginevyo hali itakuwa mbaya siku hadi siku kwa mtu yeyote nitakae amua kumfanya lolote nitakalo, na hili ni ombi langu la mwisho kwenu. Mimi ni JINI MTU” Nilisema vizuri kama msomaji wa wa habari katika  redio.

Jamaa walitishika vibaya mno hasa mkuu wa gereza la bangwe, hali ikiwa tofauti kwa yule R.P.C kidogo alionekana kuwa na chembe ndogo ya kujiamni hata akathubutu kunijibu hivi.

“Safi sana kijana, labda nikwambie hivi, kwa niaba ya jeshi la polisi, unaweza kufanya lolote utakalo amua kufanya, lakini huwezi kuwa huru dhidi ya udhalimu wako, kitendo cha sisi kunyanyua mikono juu maana yake ni kwamba umetushinda na tunakubaliana na uovu wako utakao endelea kuufanya huko mtaani, sasa hili siyo jeshi lenye mtazamo huo wa kihayawani umesikia wewe juha?”

Alisema R.P.C kwa kunong’ona hata wale maafisa wenzake walibaki na butwaa kwa vipi yule R.P.C aweze kuwa ni mwenye kujiamni kwa kiumbe kama mimi niliye kuwa zaidi ya mwanga ama mzimu.

Nilimtizama yule R.P.C nikagundua jambo katika moyo wake, ulikuwa ni moyo ulio beba ujasiri mkubwa ulionifanya niogope na mara moja nilichukuliwa na kupelekwa katika bweni moja la wafungwa,  ndani ya bweni hilo la kuishi wafungwa kulikuwa na chemba za chini kwa chini ambazo unaweza kuziita andaki.. nilingizwa katika zile chemba za chini kwa chini, ambapo huko ndani kulikuwa na chumba kimoja pweke kilicho kuwa na geti kubwa ambalo katu bila bomu usingwe weza kulivunja geti lile, humo niliingizwa na kufungiwa mule.

“Sikia kijana”  R.P.C alisema, nikiwa nakomewa kwa ndani ya kile chumba kwa makufuli imara.

“Kwa Masada tu kutoka jeshi la polisi dhidi yako ni kuwa kesi yako imefungwa bila utatuzi yanii closed but unsolved, ila wewe utaendelea kuwa kizuizini hadi hapo tume ya wataalamu maarumu itakapo amua nini hatma yako dhidi ya mashtaka haya..

Sikujibu zaidi ya  kuwatizama kwa jicho la kebehi muda wote wale maafande.

Nilitamani kuwauliza hatma ya Afande mwita na wale polisi wengine lakini sikuona umuhimu wa hilo.

Hatimae nilifungiwa katika chemba pweke kabisa, kulikuwa na hewa safi iliyo toka katika mitungi ya gesi, lakini hapakuwa na nuru  ya jua mule ndani,

Usingeweza kujua kama huu ni usiku ama huu ni mchana.,

Eneo lote lilikuwa kimya kabisa hapakuwa na japo sauti ya mbu ama kitu chochote, ilikuwa ni kama vile nipo ndani ya shimo.

Tofauti ni kuwa mule ndani kulikuwa na choo na maji, pia kulikuwa na kitanda.

Chemba hizi, mara nyingi ni chemba ambazo wanaishi watu wenye hukumu kama ya kunyongwa, ama viongozi wa nchi walio hukumiwa kwa aina fulani ya makosa katika tawala zao..

Ni magereza machache katika nchi hii ungeweza kukuta yana hivyo vitu.

Jambo moja ambalo maafande hawa hawakulijua kunifungia eneo pweke kama hili aneo ambalo lingenipa fursa kubwa ya kufanya vituko vyangu kwa uhuru mkubwa kabisa.

Usingizi ulikuwa ni kitu chenye thamani kubwa kwangu, thamani hii ndiyo iliyo nifanya niweze kuwa na madawa makali ya usingi katika maficho haya ni madawa haya ndiyo yaliyo nisadia kwa wepesi kunipeleka katika usingizi mzito , usingizi wenye kunifanya niwe kiumbe wa ajabu katika huu ulimwengu ni kiasi cha masaa takribani manne yalipita tokea niwe kifungoni kule chini ya radhi.

Nilitoa vidonge vya diazapam  na kuvitia mdomoni ambapo ilichukua kiasi cha dakika mbili kunifanya niwe katika usingizi wa ajabu na kunigia katika uwezo wangu

******

Nilismama kando ya kitanda kilicho beba kiwili wili changu kilicho kuwa kimelala usingizi wa fofofo, nikajitizama pacha ya mwili wangu na kujikuta nikitabasamu,   tabasamu la namna binadmu tulivyo fikia kiwango kikubwa cha matendo ambayo yanaweza kumfanya mtu yeyote atakae bahatika kuona ama kusikia habari za matukio haya, namna atakavyo stajabika,

Kama tu vile wewe anae soma mandishi haya anavyo stajabika!.

Nilinuia kuwa mbele ya Lody kizy, kiumbe ama jini ambaye nimepata kusikia habari zake, huku nikiambiwa ni yeye ndiye mwenye uwezo wa kujua kiini ama sababu ya mimi kuingia katika matendo haya ya ajabu kabisa

Ni hapo nilipo jikuta nipo katika eneo jipya lisilo fanana na dunia, kulikuwa na binadamu wachache lakini wengi wakiwa ni viumbe vyenye sura ya kutisha vibaya mno, haikuhitaji tution kuambiwa kuwa nilikuwa katika ulimwengu wa majini.

Lakini wakati huo huo nilikuwa mbele ya kiumbe mkubwa na mwenye sura ya kuogopesha, pengeine zaidi ya vile unavyo weza kufikilia akilini mwako.

Alikuwa ni kiumbe mwenye kichwa kama cha sokwe miguu, mikono na ngozi yake usinge weza kuitofautisha na ya tembo, alikuwa na macho madogo yaliyo ingia ndani, macho yaliyo zibwa na manyoya mengi yaliyo zunguka katika kingo za macho yake, nyuma ya mgongo wake alikuwa na mabawa makubwa kama ya popo.

Nilijikuta nimeganda bila kuelewa kama nilitingwa na uoga ama kitu gani.

Kiumbe yule alikuwa katika eneo lenye kufanana na hekalu, aliketi katika kiti chenye mwenekano wa kiti cha kifalme, pembeni yake kulikuwa na viumbe wengine wenye mwenekano wa kutisha ambao pia walikuwa ni kama walinzi wa kiumbe yule ambaye bila shaka ndiye mwenye kuitwa lody Kenzy.

Wale viumbe  walinzi wa yule kiumbe walinitizama kwa namna ya mshangao mkubwa.. vipi binadamu kama mimi niweze kufika eneo lile pasina msaada wa fulani wa majini.

Walikuwa wamejiweka tayari kwa makabiliano na mimi.

Lody Kenzy hakuwa kiumbe mwenye wasi wasi na mimi hata kidogo na alionekana kufurahishwa na ujio wangu eneo lile.

Alisimama.

Nilipo kapua macho yangu, yanii kitendo cha kufumba kope na kuzifumbua, nilijikuta ndani  ya jengo fulani ambalo sikujua ni wapi japo safari hii nilihisi nilikuwa katika dunia ya kawaida.

Nilikuwa nimeketi katika kiti cha ofisini katika eneo lenye uwazi mkubwa kama ukumbi.

Pembeni yangu aliketi jamaa mwenye asili ya kiasia akiwa katika mavazi nadhifu kabisa.

“Karibu Vegasi,. mbona umekuja bila taarifa ndugu” alisema yule jamaa tabasamu malidhawa likichanua kinywani mwake.

“Kwani wewe nani” niliuliza kwa sauti kavu.

Jamaa hakujibu badala yake alichia kicheko kikubwa kisha akasogea lile eneo la wazi, ilikuwa ni kitendo cha kujitikisa tu na mara ndani ya nukta moja, lilitokea jitu la ajabu.. jini niliye mwona muda mchache katika ulimwengu wa majini.

Kisha ndani ya nukta iliyofuata akarudi kuwa yule binadamu mwenye asili ya Kiasia.

“Lody Kezy” alisema kisha akarejea katika kiti usoni akiwa mwingi wa bashasha ya tabasamu.

“Haya sema Vegasi Mbwana, mjukuu wa Karogoyo, kituu cha Masele, mfalme wa wajenzi huru katika dunia, una nini?”

Lody Kezy alisema, huyu alikuwa ananijua zaidi ya vile nilivyo kuwa najifahamu.

“Kwanini mimi niwe mimi na….?”

“Ni zaidi ya hilo Vegasi, una mengi ya kujua, lakini labda nikuulize jambo dogo..kabla hata sijamaliza alinikatisha alikwisha jua nini nataka kujua..

“Je unafurahia kuwa binadamu mwenye uwezo mkubwa kuliko kiumbe chochote katika ulimwengu?” aliniuliza.

“Sina uhakika kama nafurahia ama sifurahii,.kwakuwa sijui lolote kuhusu hali hii,. vipi niwe mimi?”

“Nawajua binadamu ni viumbe vigeu geu mno, wengi waliopitia uongozi wa ujenzi huru walishia katika pipa la mafuta ya moto ambao walipikwa na kuliwa nyama ni kutokana na tabia za binadamu, huwezi kuwa na  nguvu za kijini kisha ukahitaji ufanye vile upendavyo wewe.. utaishi katika misingi na taratibu za kijini maadamu unategemea nguvu kutoka ujinini..labda twende katika hoja ya msingi Vegasi, nisipoteze muda wako wa kurudi katika gereza, huko uliko tunzwa kama panya buku!. Kwanini uwe wewe..”

Alisema na kuachia cheko kubwa, akibadilisha mkao katika kiti.

“Ujenzi huru haujaanza katika karne hii ya ishirini na moja, ni kiasi cha mika mingi mno ufalme huu ulikuwepo,vizazi vinapita na kuja vipya, ujenzi huru hauto koma, ni kiasi cha miaka zaidi ya tisini sasa, pamekuwa  hakuna kiongozi wa wajenzi huru kutoka katika kizazi cha Adamu na kiongozi wa wajenzi, hatokei hivi hivi tu, isipokuwa kwa sifa maalum,”

Alisema kisha akasimama na kusogea katika jokofu dogo lilikuwa mule ndani na kulifungua kisha akatoa chupa ndogo iliyo kuwa na kimiminika chenye rangi nyekundu, hata nilipo itazama vizuri nikagundua kuwa ilikuwa ni damu,   alifungua kizibo cha ile chupa kisha ‘akaigotomela’ kwa pupa kama vile anakunywa fanta ya bambucha, halafu akaendelea kusema

“Watu wenye nyota ya punda, wenye damu yenye vimelea vya anofobia wana uwezo wa kuwa viongozi wa wajenzi huru katika dunia, hutokea mara chache sana kupatika mtu mwenye sifa hizo, zaidi ya miaka tisini imepita hapakuwa na  mtu mwenye sifa hizo, hadi hapo ulipoibuka wewe,” alisema kisha akapiga funda jingine la damu, akiwa ananitizama katika mtindo wa kuuliza kama nina swali juu ya maelezo yake.

“Ilikuwaje hadi nikapatika mimi?, na vimelea vya anaofobia ni vitu gani?,” niliuliza.

“Miaka nane iliyopita palikuwa na mtu mmoja anaitwa Saumya kohil  alikuwa ni miongoni mwa wafuasi wa  wajenzi huru..” alisema Lody Kezy, nilistuka kidogo kusikia habari za Saumya kwani huyu mtu alikuwa ni mfadhili mkuu wa timu yetu ya joy ambaye kwa sasa ni mkuuu wa wilaya ya Kigoma, lakini pia ndiye mwenye jina la uficho la Ashim Azizi ambaye ni muhusika wa kifo cha mchumba wangu Nasra na mwanae, nilichukua umakini kusikiliza habari za huyu mtu.

“Huyu mtu yeye pamoja na kiongozi mkuu mmoja wa nchi moja ya huko afrika ya maghalibi ni miongoni mwa binadamu wenye sifa kuu katika falme za wajenzi huru, ni watu wanao toa kafala nzuri ya damu jambo ambalo linakuwa gumu sana kwa binadamu wengine walio katika tawala hizi..

Watu hawa wamekuwa  wepesi katika sadaka  ni kwakuwa mioyo yao imezongwa na tamaa ya mali na madalaka katika jamii zao,  hakika wajenzi huru inahitaji watu kama hawa,. Ilikuwa ni kipindi cha Saumya Kohil kutoa kafala kama ilivyo kawaida na hii ni kutokana na shukrani dhidi ya kuwezesha timu  yake kupanda dalaja na kuingia ligi kuu ya nchi…hakuwa na budi kuteketeza wachezaji wote wa timu yake katika mtindo wa ajali..ndipo hapo ulipo patikana wewe kuwa miongoni mwa wachezaji wale ambao wote walikufa isipo kuwa wewe peke yako…nafikiri kwa hilo umenielewa?”

Nilitikisa kichwa kumkubalia, kisha akendelea kusema.

“Kwa upande wa anofobia, unapo ongelea anofobia unazungumzia  kimelea kidogo sana cha njano ambacho kinakuwa katika damu ya binadamu wachache, kimelea hiki kinapandikizwa na ibirisi mkuu pindi mtoto anapo zaliwa na wazazi wake na  kuishia kuwa na majuto makubwa dhidi ya kuzaliwa kwa mtoto huyo kwa sababu moja ama nyingine”

Yule jini alisema, nilijiona kama naelea angani nikashikwa na kizunguzungu, yalikuwa ni maneno makali mno yakipenya  katika masikio yangu, lakini pia aliniongezea kitendawili kingine kikubwa kabisa.

“Vipi mimi wazazi wangu, walikuwa na majuto juu ya kuzaliwa kwangu.?” Niliuliza, huku nikijiandaa kupokea taarifa nyingine mpya yenye kuzidi kunishangaza zaidi.

Ndivyo ilivyo kuwa.

Lody Kezy alikohoa kidogo akanitizama  usoni kisha akaanza kunisimulia sababu ya msingi ya  mimi kuwa mkuu  dhidi ya jamii ya wajenzi huru.

Kila sentesi iliyo toka katika kinywa chake iliniacha na mstuko mkubwa ulio nifanya nipagawe vibaya mno.ilikuwa ni hadithi fupi lakini ya kusisimua..******

 

Je, nini kitaendelea?
Tukutane kesho hapahapa.

 

 

 

 

 

 

Leave A Reply