The House of Favourite Newspapers

JINSI YA KUJINASUA KWENYE MATESO YA MAPENZI

NI Jumatatu nyingine mpenzi msomaji wangu. Mungu ametujalia uzima, kama upo na tatizo lolote basi usikate tamaa Mungu atakufanyia wepesi na utarudi katika hali yako ya kawaida.  Kama ilivyo ada, hapa huwa tunazungumza yahu­suyo mahusiano. Tunazijadi­li kwa pamoja changamoto za mahusiano na kuzipatia majibu kwa pamoja. Kwenye ulimwengu huu wa sasa, matatizo kwenye masuala ya mahusiano yamekuwa mengi.

Usaliti umeshika hatamu, watu wana­fanya mambo bila aibu. Uaminifu umepungua hivyo kuwafanya wenza waingie kwenye mau­mivu ya mapenzi. Mtu anakuwa haridhiki, ana­kuwa na huyu huku bado anamtamani mwingine.

MAPENZI NI STAHA

Ndugu zangu, ni lazima tujifunze kwamba mapen­zi yanahitaji staha. Mapen­zi yanahitaji kujitambua na mtu kuridhika. Kuamua kwamba sasa nina uhusiano fulani basi hakuna sababu ya kuwa na mtu mwingine. Kila anayeaminiwa ana­paswa na yeye kutengeneza mazingira ya kuaminika.

Kutokana na watu wengi kutokuwa waaminifu au kuendekeza tamaa, tu­nashuhudia watu wengi wakijikuta wameingia kwenye maamuzi ambayo hawakuwahi kuyawaza. Mtu anampenda mpenzi wake lakini kutokana na vituko anavyofanyiwa, anashindwa kujizuia. Matokeo yake naye anasaliti.

TUJIFUNZE KIDOGO KWA MFANO

Rafiki mmoja aliyejitam­bulisha kwa jina la Mary, alinitumia ujumbe mfupi kunieleza kuwa anateseka sana kwenye uhusiano wake ambao hauna hata muda

ili kweli aweze kuwa mwenza wako wa maisha. Tumia kila mbinu kumbadil­isha kama kweli unampenda, usiwe mwepesi wa kukata tamaa. Jitahidi kumten­genezea mazingira ajione kwamba anachokifanya si sahihi na pengine anajid­halilisha. Ifike mahali aone kwamba anakukosea kufanya anayoyafanya bila wewe hata kutumia nguvu.

ANGALIZO

Ukiona umefanya hivyo kwa muda mrefu na makosa yamekuwa yakijirudia, anza kumuepuka taratibu. Hii ina­saidia wakati mwingine kum­fanya mtu ashtuke kwamba anapoteza mtu sahihi maishani mwake, akilibaini hilo atarudi na asipofanya hivyo basi wewe endelea na maisha yako.

Usikubali kuishi na mtu ambaye ana mambo mazito ambayo hayabadiliki. Mtu ambaye ni mhuni, malaya na ambaye hataki kubadilika kitabia haifai kudumu naye muda mrefu. Kweli muweke karibu, muele­keze taratibu lakini ukiona umefanya hivyo kwa muda mrefu na haelekei basi achana naye.

Unaweza kunifuata kwenye mitandao yangu ya kijamii, Instagram na Facebook natumia Erick Evar­ist, Twitter natumia ENangale.

Comments are closed.