The House of Favourite Newspapers

Jinsi ya Kupika Futari ya Ndizi, Nyama na Nazi

MAHITAJI

1.Ndizi mbichi

2.Nyama robo

3.Nyanya kubwa 4

4.Nazi moja kubwa

5.Kitunguu maji kikubwa 1

6.Kitunguu swaumu punje 3

7.Nyanya ya paket vijiko vya chakula 2

8.Tangawizi na kitunguu swaumu kilochotwangwa kijiko cha chakula.

MAANDALIZI

1.Osha viungo vyako vyote vinavyotakiwa kuoshwa

2.Katakata nyanya, kitunguu maji, thomu, pilipili hoho weka kwenye blenda na uvisage vyote kwa pamoja

3.Kuna nazi yako na ichuje

4.Weka tui nzito

JINSI YA KUPIKA

  1. Chemsha nyama uloiweka tangawizi kitunguu swaumu na chumvi mpaka iive.

2.Chemsha ndizi weka pembeni.

3.Weka nyanya ulizozisaga kwenye nyama yako acha baada ya hapo weka chumvi kidogo.

  1. Weka tui jepesi kwenye ndizi na chumvi acha zichemke kwa dakika tatu, usikoroge, kisha weka tui zito acha lichemke kwa dakika 2.
  2. Ukimaliza weka mchuzi wako wa nyama acha kwa dakika mbili kisha ipua acha zipoe kidogo ndio uzipakue.

Kumbuka kupika ndizi zako kwenye moto mdogo kwani ukizipika kwenye moto mkali hazitaiva vizuri na kuwa laini.

Comments are closed.