The House of Favourite Newspapers
gunners X

Jinsi ya kupika keki ya mayai, vanilla na maziwa

1

12,keki iliyokuwa imeandaliwa kwa bwana harusi na bibi harusi.Mambo vipi msomaji wangu? Wiki hii nakuletea upishi wa keki ya mayai, vanilla na maziwa. Unaweza kuandaa keki hii kwa oven au kwa rice cooker.

Mahitaji

Kikombe 1½ cha unga wa ngano (kama gramu 200)

½ kikombe cha siagi (margarine, kama gramu 133)

Mayai 2

Vijiko 2 vikubwa vya vanilla

Kikombe 1 cha sukari nyeupe (Ni kama gramu 200.)

Vijiko 1¾ vya hamira

½ kikombe cha maziwa (maziwa ya maji)

Egg-In-Tray

JINSI YA KUPIKA

Washa oven na weka kwenye nyuzi 350°F (180°C)

Paka chombo utakachotumia kuoka keki siagi (au mafuta) kwenye pande zote. (Wengi huwa wanatumia foil paper, lakini ni vizuri utumie mafuta ili upate umbo zuri la keki yako)

eggsKwenye bakuli ya wastani, weka siagi na weka sukari. Changanya pamoja. Hakikisha vimekuwa laini na vimechanganyika vizuri. (Unaweza kutumia mashine ya umeme ya kuchanganyia, lakini hata kwa mkono inawezekana.)

MAZIWAGonga mayai, changanya kwenye mchanganyiko wako. Koroga hadi yachanganyike vizuri. Weka vanilla, koroga zaidi.

Kwenye bakuli tofauti, changanya unga na hamira. Koroga vizuri ili zipate kuchanganyika kwa ufasaha.

Changanya mchanganyiko wa unga na hamira kwenye mchanganyiko wa mayai pamoja na sukari. Koroga vizuri ili vipate kuchanganyika sawia.

Weka maziwa kwenye mchanganyiko na koroga vizuri hadi iwe laini na ichanganyike vizuri.

Mwaga mchanganyiko kwenye bakuli la kuokea. Kisha weka kwenye oven. Tega muda wa dakika 40 na usubirie.

Baada ya dakika 40, toa keki, weka pembeni ipoe na kisha kata vipande ujirambe.

1 Comment
  1. Anna says

    somo ninzuri kiukweli

Leave A Reply