The House of Favourite Newspapers

Mimba kuchoropoka (Miscarriage-2)

0

1100_seven_most_common_miscarriage_causes (1)Mpenzi msomaji, leo naendelea kuelezea tatizo la mimba kuchoropoka ili uzidi kuelimika.Dalili kubwa za Miscarriage ni mama mjamzito kutokwa na damu (nzito au nyepesi) sehemu za siri kwa vipindi au mfululizo. Damu hizi hutoka kama zile zitokazo mwanamke anapokuwa kwenye siku zake na huambatana na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu.

2. Maumivu makali ya viungo
Dalili nyingine za mimba inayotaka kuchoropoka ni maumivu makali ya mgongo, kiuno, nyonga na tumbo chini ya kitovu. Maumivu haya huanza taratibu lakini huongezeka kadiri muda unavyozidi kusonga mbele. Pia huambatana na kutokwa na damu kama ilivyoelewa hapo juu.

3. Kutokwa na uchafu sehemu za siri
Dalili nyingine kubwa ya Miscarriage ni mama mjamzito kuanza kutokwa na uchafu wenye rangi sambamba na mabonge ya damu sehemu za siri.

ANGALIZO:
Dalili hizi pekee hazitoshi kuashiria kuwa tayari ujauzito umeharibika ila mama mjamzito anapoona moja kati ya dalili hizi au zote, anashauriwa kuwahi hospitali kuonana na daktari haraka iwezekanavyo.

Endapo mama atachelewa, atakuwa anajisababishia matatizo zaidi kwani sumu za kiumbe kilichoharibika huharibu mfuko wa uzazi na kusababisha matatizo makubwa siku za mbeleni ikiwemo ugumba.

KUZUIA MIMBA KUCHOROPOKA
Hakuna tiba ya moja kwa moja inayoweza kuzuia tatizo la mimba kuchoropoka ila kwa kuzingatia vyanzo vya tatizo hili, ni rahisi kuliepuka.

Kuacha tabia hatarishi
Tabia kama ulevi wa kupindukia, matumizi ya dawa za kulevya na sigara kwa wanawake wajawazito yakiepukwa, hupunguza hatari ya Miscarriage.

Kufanya mazoezi
Inashauriwa kuwa, mama mjamzito ajenga mazoea ya kufanya mazoezi mepesi angalau mara tatu kwa wiki kwa muda usiopungua nusu saa. Mazoezi kama kutembea na mengine mepesi husaidia kuimarisha misuli ya kizazi na hivyo kupunguza hatari ya mimba kuchoropoka.

Vyakula
Inashauriwa mama mjamzito kula vyakula vyenye madini ya Zinc, Magnesium, Vitamin B6 na Vitamin C kwa wingi ili kulinda ujauzito wake.
Vyakula vitokanavyo na nafaka, mimea jamii ya mikunde, karanga, kiini cha yai, mboga za majani na matunda husaidia kuimarisha afya ya mama na mtoto hivyo kuzuia tatizo hili.

Kupata chanjo
Akina mama wajawazito wanashauriwa kuhudhuria kliniki mara kwa mara kwa ajili ya kupatiwa chanjo za magonjwa hatarishi ambayo husababisha ujauzito kuharibika na kutoka.

Kupima afya mara kwa mara
Akina mama wajawazito ni lazima wajenge mazoea ya kwenda kupima afya zao mara kwa mara na kuangalia uwepo wa magonjwa kama ya zinaa na mengineyo na kama yapo watibiwe haraka ili kulinda kiumbe kilichopo tumboni.

Nikukumbushe kuwa Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume. Unaweza ukawatembelea katika vituo vyao vilivyopo nchi nzima, kwa maelezo na msaada usisite kupiga simu.

Leave A Reply