JKT QUEENS: HATUPOTEZI HATA MECHI MOJA

UONGOZI wa JKT Queens, umesema kuwa hawatapoteza hata mechi moja mpaka mwisho wa msimu kwenye Ligi ya Wanawake Tanzania inayodhaminiwa na bia ya Serengeti ili kuweka heshima kwa wapinzani wao.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Mkuu wa JKT Queens, Ally Ally, alisema kuwa wengi wanadhani timu yake ni ya kubahatisha ilihali imetwaa ubingwa hivyo ili kulinda heshima ni lazima washinde mechi zote.

 

“Tumepambana na kufi kia lengo letu la kutwaa ubingwa kama ambavyo  tulikuwa tunahitaji, sasa kazi iliyobaki ni kuendeleza rekodi ya kutofungwa mpaka mwisho wa msimu.

 

“Michezo yetu minne ambayo ipo mikononi mwetu haitupi presha  tutapambana kupata matokeo ili tushinde mechi zetu kama ambavyo tulianza ndivyo ambavyo tutamaliza,” JKT Queens wamecheza mechi 18 na kushinda zote na kujikusanyia pointi 54 kama watashinda mechi nne zilizobaki watamaliza wakiwa na pointi 66.

Na:LUNYAMADZO MLYUKA

Toa comment