The House of Favourite Newspapers

Joanita aipeleka Ijumaa Sexiest Girl, Dar Live

0

Joanitacut561Fatuma Makame ‘Joanita’.

ANDREW CARLOS
dhamini wa Shindano la Ijumaa Sexiest Girl 2015, Fatuma Makame ‘Joanita’ ambaye ni Mkurugenzi wa Hamadombe Distributor, kampuni inayodili na uandaaji na usambazaji wa filamu Bongo amependekeza mshindi akatangazwe ndani ya Ukumbi wa Dar Live siku ya Krismasi na hivyo ndivyo itakavyokuwa.

Washiriki walioingia tatu bora ni Vanessa Mdee ‘Vee Money’, Asha Salum ‘Kidoa’ na Elizaberth Michael ‘Lulu’ hivyo mshindi atakuwa miongoni mwao.

Tukio hilo litakwenda sambamba na burudani bomba kutoka kwa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ na wasanii wengine.

Akizungumzia zawadi atakayopewa mshindi, Joanita ambaye ni msanii maarufu wa filamu Bongo alisema: “Tutampa mshindi pesa, tuzo, cheti, ofa ya kufanya shopping ya nguo na kutengenezwa nywele kwa kipindi cha miezi sita.”

Leave A Reply