Kartra

Job Aandaliwa Kuisimamisha Simba

BEKI chipukizi wa Yanga, Dickson Job ambaye ni ingizo jipya kikosini hapo akitokea Mtibwa Sugar, anaandaliwa maalumu kwa ajili ya kuisimamisha Simba.Mei 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, Simba itakuwa mwenyeji wa Yanga ukiwa mchezo wa Ligi Kuu Bara.

 

Nyota huyo amekuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya nyama za paja aliyoyapata kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Gwambina FC.

 

Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa, tayari Job ameshaanza mazoezi na wenzake baada ya kupona ambapo kama ikimpendeza Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, ataanza Jumamosi.

 

“Tayari Job (Dickson) yupo fiti na kuna program maalumu amepewa kwa ajili ya kuwa fiti maana kucheza na Simba sio jambo jepesi, ikiwa mwalimu atampanga itakuwa sawa kwani ana uzoefu na mechi kubwa alizocheza alipokuwa Mtibwa Sugar na alizimudu,” ilieleza taarifa hiyo.

 

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema maandalizi yao yanaendelea vizuri, huku hali za wachezaji wao nazo zikizidi kuimarika.

LUNYAMADZO MYUKA, DAR ES SALAAM


Toa comment