The House of Favourite Newspapers

JOEL LWANGA Amwangukia Mama’ke Muna

UBUYU nao una nafasi yake kwenye jamii na ndio maana hakuna ambaye anauchukia! Baada ya mvutano wa hapa na pale kuhusiana na nani ni baba wa halisi wa mtoto Patrick ambaye kwa sasa ni marehemu na wapi msiba ufanyike, imedaiwa kuwa mpenzi wa sasa wa mama wa mtoto huyo, Rose Alphonce ‘Muna’, Joel Lwaga, amemuangukia mama yake mzazi, Ritha Moyo na Muna kumuomba radhi.

 

Chanzo chetu makini ambacho kipo ndani ya familia kilieleza kuwa, baada ya kuzuka mambo mazito kwenye mitandao ya kijamii, mpenzi huyo mpya wa Muna, ambaye ni muimbaji maarufu wa Injili alimpigia simu mama huyo akiwa Nairobi na kumuomba samahani kwa kuwa hakujua kama Muna alishaolewa kabla yake.

“Lwaga alimpigia simu mama yake Muna na kumuomba radhi kwa yote yaliotokea kwa kuwa hakuwa anajua kuwa kama Muna, alishaolewaga hivyo alimuomba wangeongea zaidi baada ya kumalizika kwa msiba wa mtoto,” kilieleza chano makini.

 

MSIKILIZE MAMA

Baada ya kupata ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimfuata mama wa Muna na kuzungumza naye alipokuwa msibani ambapo alikiri kupigiwa simu na Lwaga ila aliomba aachwe kwa kipindi hiki cha majonzi.

“Siwezi mimi sasa hivi kuzungumza chochote lakini simu alipiga (Lwaga) ila siwezi kuweka wazi kitu chochote kwa sasa,” alisema mama huyo.

 

Baada ya kuzungumza na mama huyo mzaa chema, Ijumaa Wikienda lilijaribu kuzungumza na mume halali wa Muna, Peter Zacharia ambaye alikiri kuhusu ishu ya Lwaga kumpigia simu mama yake Muna.

Ijumaa Wikienda: Kuna tetesi kuwa Joel alipiga simu na kumuomba radhi mama wa Muna kuwa hakujua kama alishaolewa na ana mume halali wa ndoa unazungumziaje hilo?

Peter: Ni kweli hata mimi nilisikia amepiga lakini mimi sikufuatilia kwa sababu na mimi nilikuwa kwenye mihangaiko ya kumpumzisha mwanangu.

Gazeti hili baada ya kuzungumza na baba wa marehemu Patrick, lilimtafuta Lwaga ambapo alipopatikana aliomba aachwe, hawezi kuzungumza chochote.

“Niachwe kwanza jamani kwa kipindi hiki siwezi kuzungumza chochote,” alisema Lwaga.

Na Imelda Mtema | Ijumaa WIkienda

Comments are closed.