The House of Favourite Newspapers

Jogoo Ashinda Kesi, Mahakama Yaamuru Alipwe Fidia

JOGOO anayejulikana kwa jina la Maurice, ameshinda kesi iliyokuwa inamkabili nchini Ufaransa ambako alikuwa anashtakiwa na majirani zake kwa kuleta usumbufu wa kupiga kelele wakati wa asubuhi (kuwika) wakitaka ahame katika maeneo waliyopo.

Mahakama imeamuru Maurice alipwe fidia ya Euro 1,103 sawa na Shilingi milioni 2 za Tanzania kama usumbufu ambao ulisababishwa kutoka kwa majirani ambao walianza kumshtaki kuanzia mwaka 2017.

Mwanasheria wa jogoo huyo amesema, kuku ni ndege asiye na hatia,  ni jambo la kipuuzi kuona watu wanamshtaki kutokana na alivyofanya. Aidha mmiliki wa jogoo huyo amesema ushindi wa kesi alioupata dhidi ya jogoo wake ni ushindi wa kila mtu, na atakuwa ni mfano wa viumbe wengine duniani kote.

Pia uongozi wa juu nchini Ufaransa umesema viumbe kama Maurice wanatakiwa wapewe heshima na wawekwe katika nyumba ya makumbusho kwani anawakilisha nembo ya taifa lao.

Wanyama na wadudu wengine walioshtakiwa kuhusu suala la kupiga kelele nchini Ufaransa ni mbuzi, ng’ombe, nzige (balale) p na kengele ya kanisani.

Comments are closed.