Waliooa FC waitungua Wasiooa FC – Pichaz

Saleh Ally (kulia) wa Waliooa FC akiwa na wachezaji wengine wakati mechi ikiendelea.

   

HATIMAYE ule mpambano wa karne kati ya timu ya Waliooa FC dhidi ya Wasiooa FC zote za Makampuni ya Global Group, umepigwa jana Ijumaa, Septemba 6, 2019, katika Uwanja wa CCM, Sinza, jijini Dar es Salaam huku Waliooa FC wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Philip Nkini wa Waliooa FC na Ally Mbetu wakiwa kazini.

Mechi hiyo iliyokuwa na ushindani wa aina yake ilianza majira ya saa 10:00 huku timu zote zikiwa zimekamiana na kila mmoja akiwa na uchu wa kuchungulia nyavu za mwenzake.

Wasiooa FC walianza kwa kasi huku wakilisakama lango la Waliooa FC mara kwa mara lakini kwa umaridadi wa kipa wa Wasiooa FC, ilikuwa ngumu kwani alikuwa akiokoa michomo kama de Gea vile.

Mambo yalianza kubadilika kuanzia dakika ya 20, ambapo Waliooa FC walishika kasi na kurejea mchezoni rasmi, hali iliyowashangaza mashabiki wengi wa timu hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wao, Eric Shigongo.  Walilisakama lango la Wasiooa  kama nyuki na kunako dakika ya 35, Walioa wakafanikiwa kupata bao la kwanza kupitia kwa Hamisi bao ambalo lilidumu kwa kipindi chote cha kwanza.

Waliooa FC wakiwa mapumziko.

Kipindi cha pili kilikuwa vilevile, Waliooa FC walifanya mabadiliko wakimtoa Mbrazil, Santosh, Amran Kaima na Saleh Ally Jembe, na nafasi zao kuchukuliwa na Ally Mbetu, Borry Mbaraka na Deo, mabadiliko ambayo yaliiongezea nguvu mpya timu hiyo.

Wilbert Molandi (Waliooa FC jezi ya blue) akimtoka Marco Mzumbe.

Dakika ya 65, Waliooa  walifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Wilbert Molandi ‘Momo’ baada ya kutokea piga-nikupige iliyosababishwa na mpira wa adhabu langoni mwa Wasiooa FC na kujihakikishia ushindi huo mnono na wa kihistoria.

Beki Edwin Lindege ‘Marcelo’ akihakikisha ulinzi.

Dakika ya 70, Wasiooa FC walizinduka kutoka katika usingizi wa pono waliokuwa wamelala, na kuanza kulisakama tena lango la Waliooa FC. Dakika ya 84 walifanikiwa kupata mpira wa adhabu baada ya mchezaji wao Abdul kufanyiwa madhambi nje ya 18.

Saleh akitoa maelekezo kwa vijana wake.

Mpira huo wa adhabu ulipigwa na Said Omary na kuzama moja kwa moja wavuni, hivyo kuwaandikia Wasiooa FC bao la kufutia machozi, mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa, Waliooa FC 2-1 Waliooa FC.

Ally Mbetu akiachia mkwaju.

Timu ya Wasiooa FC ipo chini ya udhamini mnono wa Kessy Marketing Agency na Waliooa FC imedhaniniwa na Saleh Jembe Blog.

 

 

Amrani Kaima akifanyiwa ‘sub’.

Na Edwin Lindege.


Loading...

Toa comment