The House of Favourite Newspapers

Joh Makini Alivyoifungukia… Perfect Combo

1

Joh-makini.jpgJohn Simon Mseke ‘Joh Makini’.

ANDREW CARLOS

MTAYARISHAJI, mwongozaji na mwanakatuni maarufu wa Kimarekani, Walter Elias Disney ‘Walt Disney’ aliyewahi kutamba na katuni za Mickey Mouse, Minnie Mouse na Pluto mara kwa mara alikuwa akitumia msemo wa kuwapa watu njia za kutoboa (kufanikiwa) kwa kusema; ‘Ndoto zote unazoota huwa ni za kweli kama tu utazifanyia kazi.’

Msemo huo naufananisha na anachokifanya sasa staa wa Muziki wa Hip Hop Bongo, John Simon Mseke ‘Joh Makini’. Joh ni mmoja kati ya marapa wakubwa nchini akiwa na ngoma kibao kama Mfalme, Wameinama, Stimu Zimelipiwa, Zamu Yangu, Chochote, Manuva, Najiona Mimi, Karibu Kwenye Show za Joh, OX,Nusu Nusu na nyingine kibao.

Chidinma EkileChidinma

Hadi sasa anaendelea kutimiza ndoto zake za kutoboa kimataifa kwani ameshafanya kolabo mbili, moja na staa wa Sauz, AKA na ya pili kutoka kwa staa wa Nigeria, Chidinma.

Ikumbukwe Joh hakuwa na ndoto za kukutana ghafla na AKA lakini kilichotokea, mwaka jana akiwa mmoja kati ya waalikwa katika shoo ya mpenzi wa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zari iliyojulikana kama Zari All White Party alikutana na AKA na kufanya mipango ya Wimbo wa Don’t Bother unaoendelea kutikisa Afrika hadi sasa.

Mwaka juzi pia nchini Kenya, Joh aliingia kwa mara ya kwanza katika shoo ambayo hukutanisha mastaa mbalimbali Afrika na kuimba wimbo pamoja ambapo alipangiwa na staa wa Nigeria, Chidinma na kuimba naye Wimbo wa Najiona Mimi.

Baada ya kumaliza shoo hiyo, Joh alitimiza ndoto za kukutana na Chidinma kwa kugonga naye ngoma hukohuko nchini Kenya na ngoma hiyo ni Perfect Combo inayotikisa kwa sasa.

Katika makala haya, Joh anafungukia muziki wake kwa ujumla hadi alipo sasa;

Over Ze Weekend: Wimbo wako wa Perfect Combo una maanisha nini?

Joh: Neno Combo kwanza ni kifupi cha Combination yaani muunganiko. Perfect Combo nilikuwa namaanisha wapenzi wale wanaoshibana, wanaokerana na kugombana lakini mwisho wa siku wanarudiana na kuwa kitu kimoja.

Over Ze Weekend: Umewezaje kumuimbisha Chidinma wa Nigeria lugha ya Kiswahili?

Joh: Ujue Tanzania tunapata bahati sana ya kufanya ngoma za kimataifa na tunapopata shavu hilo ni lazima tulitumie ipasavyo kutangaza lugha yetu kama tunavyotangaza milima na mbunga. Nilikuwa na ndoto za kumuimbisha Chidinma Kiswahili na hilo limetimia kwani naamini alivyoimba kuna Wanigeria wenzake nao wanafurahi kumsikia akiimba lugha hii.

Over Ze Weekend: Perfect Combo audio ameitengeneza nani?

Joh: Ngoma ilipikwa mwaka juzi na Prodyuza R Kay maarufu nchini Kenya ambaye ameteng-eneza hits kibao kama Gentleman ya P Unit wakishiri-kiana na Sauti Sol.

Over Ze Weekend: Inaonekana kama kundi lenu la Weusi (G.Nako, Bonta na Nikki wa Pili) lipo kimya sana kila mmoja anatoa kazi kivyake, lini mtaungana?

Joh: Mi naona bado tupo kama kundi maana kila ngoma inayotoka iwe ya Nikki au G Nako lazima wote tutashirikiana kuanzia inatengenezwa audio hadi video na kwenye shoo pia so kazi yangu ni ya Nikki pia ni ya G Nako.

Over Ze Weekend: Umeshafanya shoo yoyote kubwa Sauz au Nigeria?

Joh: Bado kiukweli ila Mungu akipenda soon itakuwa hivyo.

Over Ze Weekend: Kwa jinsi ulivyoona Hip Hop ya Ghana, Sauz na Nigeria zinaonekana zipo juu kwa Afrika, sisi tunakosea wapi hadi?

Joh: Hip Hop ya Bongo ni nzuri kuliko yoyote Afrika. Tuna hazina kubwa ya vipaji na audio tuko juu. Utofauti wao walianza mapema na sisi tumekuja kushtuka hivi karibuni. Video zetu zamani hazikuwa bora lakini sasa ni bora.

1 Comment
  1. filbert mapendo says

    Much respect to u ..joh

Leave A Reply