The House of Favourite Newspapers

JOHARI: Naogopa Kupangwa Msururu!

0
Blandina Chagula ‘Johari’.

JINA la Johari si jina geni kwa wapenzi na wadau wa sanaa Bongo kutokana na kuifanya sanaa hiyo ilipokuwa chimbuko lake ni makundi, mrembo huyu ambaye jina lake halisi ni Blandina Chagula, alichipukia kupitia Kundi la Kaole Sanaa Group.

Johari ambaye sura yake imepamba filamu nyingi za Kibongo, licha ya umri kuonekana kumtupa mkono, amesema hadi sasa bado hajampata mwenza ambaye ataweza kumnadi na kumuonesha lakini Mungu akimpatia atafanya hivyo.

SHOWBIZ XTRA: Vipi Johari umepoa sana, mpaka sasa wameibuka watu wengine wameweza kufunika jina lako kabisa unafikiri ni kwa nini?

JOHARI: Unajua siku zote avumae baharini ni papa kumbe wengine wapo, mimi sibabaishwi na waliokuja hivi sasa kwa sababu natambua vizuri kabisa jinsi ninavyofanya kazi kwa maana mimi ni mtunzi, muongozaji mara nyingi kwa sasa nakaa nyuma ya kamera tu.

SHOWBIZ XTRA: Sasa hivi ni kama soko la filamu limeporomoka lakini bado naona unaendelea kukomaa unafanyaje ili kukabiliana na hali hiyo?

JOHARI: Unajua siku zote ni kujipanga tu na kuhakikisha kitu unachokitoa ni bora hata kikienda kwa mtazamaji anaikubali kweli ni kazi nzuri.

SHOWBIZ EXTRA: Kipindi cha nyuma Johari ilikuwa ni nadra sana kuonekana ukijumuika na wenzako kwenye ishu mbalimbali za sanaa lakini sasa hivi nakuona ni mstari wa mbele nini kimekuhamasisha?

JOHARI: Nafikiri kila jambo na wakati wake zamani kulikuwa na kazi nyingi sana za kutengeneza filamu na tulikuwa hatuwezi kutoka wote tukaacha ofisi wazi.

SHOWBIZ XTRA: Mastaa wengi wamekuwa wakiweka wazi mahusiano yao ya kimapenzi wazi vipi kwa upande wako mbona unayaficha?

JOHARI: (kicheko) Siyo kama nayaficha lakini bado sijampata mtu sahihi wa kumnadi kwa watu maana nitakuwa naonyesha mtu kesho tumemwagana halafu na mimi nikaingizwa kwenye listi ya wasanii wenye msululu wa wanaume.

SHOWBIZ XTRA: Kwa hiyo mpaka sasa huna mpenzi?

JOHARI: Na ndio maana kila siku namuomba Mungu anipe na mimi wa kwangu najua atajibu tu maombi yangu.

SHOWBIZ XTRA: Hivi ni kweli una mtoto?

JOHARI: Mbona ninaye mtoto kwani hamjui?

SHOWBIZ XTRA: Umezaa na nani?

JOHARI: Mtu niliyezaa naye ndio siwezi kumuweka wazi ila wewe elewa tu mtoto ninaye.

SHOWBIZ XTRA: Mbona inasemekana yule ambaye mara kadhaa ulimnadi mitandaoni na kwenye vyombo vya habari si mwanao bali ni mtoto wa mdogo wako?

JOHARI: Mimi ndio nakuambia sasa yule ni mwanangu, sasa sijui utamuamini nani mwingine.

SHOWBIZ XTRA: Kumekuwa na madai siku hizi umekuwa mtu wa kilevi sana mpaka umepitiliza vipi kuhusu hilo?

JOHARI: Sidhani kama kuna ukweli kuhusu hilo lakini hata hivyo hakuna mtu anayemzuia mtu kufanya kitu akipendacho.

SHOWBIZ XTRA: Una kitu kingine unatarajia kufanya zaidi ya filamu?

JOHARI: Ndio kuna biashara najipanga nataka kufanya kama ikikamilika nitaiweka wazi tu.

SHOWBIZ XTRA: Asante sana Johari nashukuru sana kwa ushirikiano wako.

JOHARI: Karibu sana.

 Makala: IMELDA MTEMA | IJUMAA WIKIENDA

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave A Reply