The House of Favourite Newspapers

JOHN HECHE AUNGANISHWA KESI YA AKINA MBOWE

MBUNGE wa Tarime Vijijini (CHADEMA), John Heche amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Aprili 5, 2018 kisha kusomewa mashtaka matatu yakiwemo ya uchochezi wa chuki kwa wananchi dhidi ya serikali iliyoko madarakani.

 

Heche ambaye alijisalimisha polisi na kushikiliwa tangu juzi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, anadaiwa kutenda makosa hayo akiwa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Buibui Kinondoni, jijini Dar es Salaam, mnamo Februari 16, 2018.

 

Heche na wenzake saba ikiwa ni pamoja na Mbowe, anadaiwa kufanya mkusanyiko usio halali na uliopelekea maandamano na vurugu zilizosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini na askari polisi kujeruhiwa, Feb. 26.

 

Baada ya kusomewa mashataka hayo, Heche ameunganishwa katika kesi inayowakabili viongozi wengine saba wa Chadema waliosota rumande kwa siku saba katika Mahabusu ya Segera na kupewa dhamana juzi Jumanne katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutimiza masharti.

 

Wengine wanaoshtakiwa katika kesi hiyo ni Vincent Mashinji, John Mnyika,  Salum Mwalimu, Ester Matiko, Mch. Peter Msigwa na Halima Mdee.

Maaskofu Mnacheza Mchezo Katika Dini – Riziki Lulida

Comments are closed.