The House of Favourite Newspapers

John Legend kupata mtoto wa kike

0

chrissy-teigen-pregnant-modStaa wa muziki wa R&B, John Legend akiwa ameshika tumbo la mkewe (Chrissy).

KAMA ulikuwa unajiuliza kama staa wa R&B, John Legend anayetamba na Ngoma ya All of Me atapata mtoto wa kike au wa kiume, jibu umeshalipata baada ya juzi kati kuweka wazi.

Mezzanine_502

John Legend akiimba moja ya nyimbo zake jukwaani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, John Legend ambaye anaishi na mkewe, Chrissy Teigen aliweka wazi jina la mtoto na hiyo ilikuwa baada ya kufanyiwa mahojiano na Jarida la Vogue toleo la Thailand.

people-john-legend-20315281jpg

John Legend akipigwa busu na mkewe (Chrissy).

Akizungumzia hisia zake juu ya mtoto wake huyo mtarajiwa, John Legend alisema;

“Najivunia kuheshimika kwa kuchukua vipande vya kava jipya la Vogue. Pia najivunia kuwepo kwa toleo hili la Thai, baada ya kupiga picha hizi nimegundua kitu kuwa kati ya mimi na mke wangu (Chrissy) tunatarajia kuwa na mtoto wa kike.”

Imetayarishwa na Andrew Carlos/GPL

Leave A Reply