The House of Favourite Newspapers

Jokate Aapishwa Kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe

 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto),  akimwapisha Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.
Mwegelo akisani kiapo.

Mkuu mpya wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ameapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, akichukua nafasi ya Hapiness Seneda huku akipewa onyo kuepuka wapotoshaji. Pamoja na Jokate, Zainab Kawawa naye ameapishwa kuwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo.

 

Jokate, ambaye aliwahi kuwa mlimbwende wa mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2006, aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Julai 28 mwaka huu.

 

Akizungumza mara baada ya wakuu hao wawili wa wilaya kuapishwa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani, Ramadhani Maneno amewataka wateule hao waepuke wanaofika ofisini kutaka kuwapotosha katika utendaji wao.

Amewataka wakakae na makatibu tawala ili wakusanye mapato kwani mkoa wa Pwani una viwanda.

 

“Kwa nafasi mlizopata hakikisheni mnakua karibu na viongozi wa chama hilo ni jambo kubwa. Wakati sasa mnaenda kuripoti kwenye wilaya mkaanzie kwenye ofisi za chama,”amesema.

 

Ameongeza “Huko mnapoenda mtafute desturi na mila za maeneo yenu msizipuuzie, lakini mtafute yale yanayoendana na nyaraka zilizopo.”

 

Amesema anawakabidhi vitu vitatu, macho, masikio na mdomo ambavyo vitawasaidia kwenye utendaji wao wa kazi.

Comments are closed.