The House of Favourite Newspapers

Jokate ateswa na skendo!

1

jokate12Stori: Boniphace Ngumije

DIVA mwenye jina kubwa kwenye Tasnia ya Mitindo na Urembo Bongo, Jokate Mwegelo amefunguka kuwa miongoni mwa mambo ambayo huwa yanamkosesha raha ni kusikia akihusishwa kwenye skendo hasa zinazomchafua na kufanya watu ndani ya jamii kumchukulia tofauti kitabia.

Jokate ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na Uwazi Showbiz na kuongeza kuwa mbali na yeye kumtesa pia familia yake huwa haifurahii kabisa skendo hizo na hupata wakati mgumu kuwaeleza nini kinakuwa kinaendelea kila anapokwaa skendo.

“Kiukweli skendo zinazonichafua huwa zinanitesa sana, unajua mimi bado mdogo na ninatakiwa kuandaa maisha yangu ya kesho, sasa ikiwa hiyo kesho watu wakinifahamu kwa mabaya ni wazi hata nikihitaji msaada wao pengine unaohusu masuala ya kijamii hawatanielewa,” alisema Jokate.

1 Comment
  1. Mary berege says

    Unajitakia mwenyewe mara kuwa na huyu mara huyu unafikiri ni vzr? Ulikuwa ukiimba kwaya ya mt petro nasikia ss umeacha wacha uandamwe na skendo na mavazi yako ya utupu ndiyo yanakuponza bi mdada jisitiri ndg

Leave A Reply