The House of Favourite Newspapers

Fahamu madhara ya asali

1

asaliAsali  hutengenezwa na nyuki wanaotumia ‘vumbi’ maalum la maua liitwalo nectar.  Kiwango cha sukari katika asali ni asilimia 70 hadi 80 na kiasi kinachobaki ni maji, madini na huwa na kiwango cha protini, asidi na vitu vingine.

Asali imekuwa ikitumika kwenye matibabu ya vidonda, matatizo ya ngozi na magonjwa tofauti ya tumbo na ina uwezo wa kuua bakteria mwilini.

Pamoja na uzuri na utamu wa asali lakini ina madhara yake kwani inaweza kuongeza uwezekano wa kutokwa damu, ikiliwa pamoja na dawa zinazoyeyusha damu kama vile Asprini, dawa za kuzuia damu kuganda kama Warfarin(Coumadin), Heparin na kadhalika.

 Asali pia inaweza kushusha kiwango cha sukari mwilini, hivyo lazima kuwe na tahadhari ya matumizi yake kwa mtu mwenye ugonjwa wa kisukari anayetumia dawa zinazoshusha sukari mwilini kwa sababu zikitumika kwa pamoja huweza kusababisha kushuka sana kwa sukari na kuleta hatari ya kifo au kifafa kwa mtumiaji.

 Asali pia inaweza kushusha shinikizo la damu mwilini, hivyo wagonjwa wanaotumia dawa za kushusha shinikizo la damu la juu (High Bloodd Pressure), wanapaswa kushauriana na madaktari wao kabla ya kutumia.

 Asali pia inaweza kuingiliana na dawa zinazofanya kazi kwa kutumia kimeng’enya mwili cha Cytochrome p450 kinachofanya kazi  ya kuvunja dawa na hivyo huweza kufanya dawa ifanyekazi kwa kiwango kidogo ama kufanya kazi kwa kiwango zaidi ya kile kilichokusudiwa hivyo kuwa sumu ama kutomsaidia mtu. Mtu anayetumia dawa hizo anatakiwa kuongea na mtaalam wa afya ili amueleze kama ni salama kunywa dawa zinazohitaji kimeng’enya hiki katika utendaji kazi mwilini pamoja na asali kwa usalama wao.

 Asali pia inaweza kuingiliana na dawa za damu, moyo, mfumo wa fahamu, ngozi, tumbo au matumbo, fangasi, mfumo wa mkojo, saratani, kifafa, kupunguza lehemu, meno, pombe, kupunguza uzito na dawa za kutibu vidonda.

 Asali inaweza kuwa na mzio kwa baadhi ya watu hivyo inawabidi wasitumiwe. Watu hao wakila asali wanaweza kukohoa, kuwa na pumu, kuvimba chini ya ngozi, kupungukiwa/kuishiwa pumzi na kadhalika. Ukiwa na matatizo hayo muone daktari kabla ya kula asali kwani pia inatakiwa isitumiwe pamoja na dawa za asili zinazofanya kazi kama nilizotaja hapo mwanzoni kama za kushusha shinikizo la damu na sukari mwilini.

1 Comment
  1. mzizimkavu says

    Yote hayo uliyo yasema bado haijawa kuw aAsali ina madhara:Huwezi kufananisha Dawa za Sumu za hospitali na Asali ni vitu 2 tofauti umetaja madhara ya asali lakini hujataja faida zake Asali. Bado mimi sijakubaliana na maelzo yako hayaja nitosheleza endelea kuzidi kufafanuw anipate kuelewa zaidi asante.

Leave A Reply