The House of Favourite Newspapers

Jose Chameleon Naye Atua Bongo Kupiga Shoo Ya Oktoba Fest Ya SBL Coco Beach Kesho

0
Jose Chameleon baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo usiku kwaajili ya shoo ya kesho Jumamosi Ufukwe wa Coco.

Dar es Salaam 20 Oktoba 2023: Msanii mkongwe wa muziki muziki kutoka nchini Uganda, Jose Chameleon jioni ametua hapa nchini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya kupiga shoo ya Oktoba Fest iliyoandaliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries.

 

Chameleon akipoza koo baada ya kutuwa uwanja wa ndege.

Chameleon ameungana na msanii mwenzake Nyanshiski kutoka nchini Kenya ambaye aliwasili hapa nchini leo asubuhi kupitia uwanja huo wa ndege wa kimataifa kwa ajili ya kufanya shoo ya hiyo ambapo mwanamuziki Ali Kiba naye anatatarajiwa kufanya makamuzi kwenye shoo hiyo.

Akizungumza na wanahabari waliofika kumpokea uwanjani hapo Chameleon amesema hana maneno mengi ameitwa kwa ajili ya kazi na atakachofanya ni kuhakikisha anapiga kazi kama kawaida yake na kuacha gumzo.

Leave A Reply