The House of Favourite Newspapers

JPM AKUTANA NA PRINCE WILLIAM WA UINGEREZA

Rais  John Magufuli akisalimiana na mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William, alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo.
…Akiwa katika mazungumzo na Prince William aliyeambatana na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke, Wengine ni Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla akiwa na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi.
…Akimkabidhi Prince William picha ya wanyama wanaopatikana katika mbuga mbalimbali hapa nchini.

 

…Akimkabidhi Kamusi ya Kiswahili.
…Akipokea zawadi kutoka kwa Prince William inayomwonesha Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akizungumza na Malkia wa Uingereza, Elizabeth II.

 

 

Wakiagana.  

(Picha na Ikulu, Dar es Salaam)

Rais  John Magufuli leo amekutana na mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William, Ikulu jijini Dar es Salaam na kufanya naye mazungumzo ambapo baadaye walipeana zawadi mbalimbali.

Comments are closed.