JPM Amtumbua RC Kebwe, Ateua Mwingine – Video

RAIS John Magufuli amemteua Lowata Sanare kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Musa Masele kuwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Morogoro.

 

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Charles Kabeho, amehamishiwa Chato,  na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Msafiri Mtemi amehamishiwa Wilaya ya Tarime.

 

Aidha, Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi 12 watakaowakilisha Tanzania nchi mbalimbali, ambapo katika uteuzi huo wamo pia Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Benson Bana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dkt. Modestus Kipilimba.

 

Walioteuliwa kuwa Mabalozi ni:

1. Mohamed Mtonga
2. Dkt. Jilly Maleko
3. Dkt Benson Bana
4. Meja Jen. (Mst), Anselimu Bahati
5. Prof. Emmanuel Mbennah
6. Maimuna Tarishi

7. Meja Jen. (Mst) Gaudence Milanzi
8. Ali Jabir Mwadini
9. Dkt Modestus Kipilimba
10. Jestas Nyamanga
11. Prof. Dr. Kennedy GASTORN
12. Mhandisi Aisha Amour.


Toa comment