Kwanini Trump Anabeba Pesa Mfukoni

Wakati akipanda ndege kuelekea  California, Rais Trump wa Marekani alipigwa picha zikimuonyesha kuwa na noti nyingi za dola 20 zilizoonekana kwenye mfuko wake wa nyuma.

 

Baada ya kurejea Washington, wanahabari walimuuliza rais Trump kuhusu picha hiyo na kama ni utaratibu wake kubeba pesa taslimu mifukoni mwake ambapo alikubali na kulitoa burungutu la pesa mfukoni mwake kisha kuwaonyesha wanahabari.

“Siwezi kubeba ‘waleti’ kwasababu sina haja ya kutumia ‘credit card’ kwa muda mrefu sana. Napenda sana kuwapa wahudumu wa hoteli sehemu ya chenji ninazobakiza. Nawaambia ukweli, au rais hapaswi kufanya hivyo?”, lakini mimi ninapenda.” alijibu Trump.

 

Rais Donald Trump ambaye amekuwa haishiwi vituko, alitumia muda wake kumpongeza mpiga picha na kuomba nakala ya picha hiyo.

Toa comment