The House of Favourite Newspapers

JPM Amwaga Mamilioni 5 kwa Wanakijiji wa Mkula, Morogoro – Video

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amekabidhi kitita cha Tsh. Milioni 5 kwa wanakijiji wa Mkula, Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya ujenzi wa shule katika kijiji hicho huku akisisitiza kuwa ataendelea kuwasaidia wananchi wake kutatua changamoto zinazowakabili na kuboresha miundombinu mbalimbali.

 

Magufuli ambaye yupo ziarani mkoani humo amekabidhi pesa hizo leo Mei 5, 2018 na kupokelewa na viongozi  wa kijiji hicho kwa naiaba ya wananchi wote huku akiwataka wasizitafune badala yake zikatekeleze mradi uliokusudiwa na yeye atafuatilia kujua iwapo zimetumika kama ilivyokusudiwa.

 

Rais Magufuli ameyafanya hayo akiwa njiani kuelekea wilayani Kilombero, ambapo atazindua daraja la Mto Kilombero, ambapo wananchi wa kijiji hicho waliusimamisha msafara wake na kuzungumza nae wakimuelezea na kero zinazowakabili zikiwemo za huduma za afya.

SHUHUDIA RAIS MAGUFULI AKIMWAGA PESA HIZO

Comments are closed.