JPM Ashuhudia Viboko Hifadhi ya Katavi – Video

RAIS  John Magufuli ameonyesha kwa vitendo maana ya utalii wa ndani kwa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi.

Amtembelea hifadhi hiyo jana Jumatano, Oktoba 9, 2019 na kupata wasaa wa kuzungumza na wahifadhi ambapo aliwapongeza kwa kazi nzuri ya kuhifadhi wanyamapori na kukabiliana na ujangili, hali iliyowezesha kuongezeka kwa idadi ya wanyama wakiwemo waliokuwa hatarini.

Rais aliwasisitiza wahifadhi hao kuhusu umuhimu wa kutunza maliasili za taifa.

“Wapo wenzenu wachache wanaoshirikiana na majambazi, waache;  na wakipatikana wa namna hiyo, peleka mahakamani wafunguliwe kesi ya uhujumu uchumi,” alisema.

TAZAMA TUKIO HILO HAPA


Loading...

Toa comment