The House of Favourite Newspapers

JPM Awapongeza Wanawake Nchini, Serikali Kuendelea Kuwathamini

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amesema kuwa Serikali yake itaendelea kuwathamini na kuwaheshimu wanawake na kuwajengea mazingira bora, ambayo yatawarahisishia katika kutekeleza majukumu yao.

Hayo ameyabainisha leo Machi 8, 2020, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, wakati akituma salamu za pongezi za kuwatakia heri wanawake wote katika kuadhimisha siku ya wanawake Kimataifa, inayosherehekewa duniani kote.

“Nawapongeza Wanawake wote kwa kuadhimisha siku hii muhimu, mchango wenu kwa familia, jamii na Taifa hauna mfano, Serikali ninayoiongoza itaendelea kuwathamini, kuwaheshimu na kujenga mazingira bora, yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yenu ipasavyo” amesema Dkt Magufuli.

Leave A Reply