The House of Favourite Newspapers

JPM Igunga: Bilioni 1 Mnajenga Mitaro?…. Naondoka – Video

RAIS John Magufuli amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga mkoani Tabora,  Revocatus Kuuli,  kuitisha kikao haraka na madiwani na kujadili nao kisha kupanga upya matumizi ya pesa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja zilizotolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo ya wilaya hiyo.

 

Magufuli ametoa kauli hiyo leo Novemba 27, 2019, katika eneo la Shelui wilayani Igunga mkoani Tabora akiwa njiani kuelekea Shinyanga baada ya Kuuli  kumueleza kuwa zaidi ya Tsh bilioni 1 zilizotolewa na Serikali zimeelekezwa kwenye ujenzi wa mitaro na kuboresha miundombinu ya halmashauri hiyo.

 

“Mngekuwa na madiwani wazuri mngentengeneza barabara hapahapa lakini wao wamepitisha bilioni 1.5 kwa ajili ya kutengeneza mitaro. Nakuagiza Mkurugezni itisha kikao kesho na madiwani wote, mpange upya matumzi ya pesa hizo, mchague barabara hata moja ama mbili hapa mjenge kwa lami, haiwezekani pesa itolewe na serikali kuu, zaidi ya bilioni moja halafu madiwani wanapitisha kujenga mtaro kwa sababu mnawapa posho, ni aibu.

 

“Mkurugenzi na diwani simamieni hilo, vinginevyo nitatoa maamuzi hizo pesa zisije hapa, pesa za walipa kodi haziwezi kuja hapa kutengeneza mitaro tu….. Sasa naondoka mambo mengine yanaudhi. Uzuri hapa ni barabarani, nitapita siku moja hapa nitaona, ole wenu mfanye yenu,” alisisitiza.

 

Aidha amewaahidi wananchi wa eneo la Shelui mkoani Tabora, kufikia Januari mwaka 2020 kuwapelekea fedha Sh milioni 200 kwa ajili ya kujenga kituo cha afya. Fedha hizo ziliahidiwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wakati Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi.

 

“Rais Kikwete aliahidi na ahadi ikiahidiwa lazima itekelezwe, hapa lazima pawe na kituo kikubwa cha afya, hizo Sh milioni 200 na mimi nitaongeza zitakuwa 250 nitazileta hapa, wajenzi watakaotumika wasichakachue, ole wao waje wajaribu kufanya hivyo!”

MSIKILIZE JPM AKIWA TABORA

Comments are closed.