The House of Favourite Newspapers

JPM: Kama Mkandarasi ni Mshenzi Mimi ni Zaidi Yake – Video

KATIKA mwendelezo wa Ziara yake Kanda ya Ziwa, Rais John Magufuli leo Septemba 5, 2018 amefanya ziara katika wilaya ya bunda, mkoani Mara na kuibua mambo kadhaa ikiwemo kusimama kwa mradi wa maji na matatizo ya ardhi kwa wananchi.

 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bunda, Abraham Magese ametoa malalamiko kwa Rais Magufuli kwamba licha ya Waziri Mkuu kumtumbua Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Musoma na kuvunja Bodi hiyo, lakini mradi wa maji wa Tsh. 16b bado haujakamilika Bunda.

 

Akitatua kero hiyo Rais Magufuli amemhoji Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima kuhusu hatua walizochukua ili kukamilisha mradi huo baada ya Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Muwasa asimamishwe na Bodi hiyo ivunjwe.

 

“Tangu Januari Waziri Mkuu alipoondoka hapa bado mnawachunguza tu mpaka leo, wananchi hawana maji? Kwa nini mkandarasi usimsondeke hata ndani? Nauhakika Baba wa Taifa Mwl. Nyerere angetokea leo akakuta kuna mradi wa maji haujakamilika kwa miaka 8 Bunda, angeshangaa sana. Angeishangaa Serikali yangu, Mkandarasi na wale walimlipa huyo mkandarasi. 

 

“Kama wanabebana kiundugu wataachiana, hili suala la Maji Bunda nimelibeba mimi mwenyewe, sasa naomba mniachie, kama Mkandarasi ni mshenzi basi mimi ni mshenzi zaidi. Kama ni kutumbua mimi nitatumbua, kama ni kufukuza nitawafukuza, kama hawakutubuliwa siku za nyuma mimi nitawatumbua kinyumenyume, ninataka Mkuu wa Mkoa ufanye kazi,” amesema Rais Magufuli.

VIDEO: MSIKIE RAIS MAGUFULI AKIZUNGUMZA HAPA

Comments are closed.