The House of Favourite Newspapers

Kim Kardashian Apuuza Uvumi wa Kutembea na Drake

STAA mtangazaji wa televisheni wa Marekani,  Kim Kadarshian amepuuza  uvumi uliozagaa kwamba ana uhusiano wa siri wa kimapenzi na rapa Drake.

Uvumi huo umetokana na mtumiaji mmoja wa mtandao wa Twitter, @tmorrison24, aliyesema alinasa ujumbe unaoonyesha kuna kitu wawili hao wanamficha  Kanye West, mume wa Kim.

Mtumiaji huyo alisema ujumbe huo ulitokana na wimbo wa Drake wa “Scorpion”  ukiwa na maneno Kiki do you love me,  ambapo alidai Kiki ni jina bandia la Kim.

Hata hivyo, Kim amepuuza uvumi huo na ku-post ujumbe kwenye Instagram usemao: “Never happened. End of story.”  yaani “Kamwe halikutokea hilo.  Mwisho wa stori.”

Comments are closed.