The House of Favourite Newspapers

JPM Kupokea Dreamliner Nyingine Mpya Leo

Ndege mpya ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, iliyonunuliwa na Serikali imeondoka nchini Marekani jana Ijumaa, Oktoba 25, 2919 kuja Dar es Salaam Tanzania.

Ndege hiyo kubwa yenye uwezo wa kubeba abiria 262 inatarajiwa kutua katika Uwanja wa N dege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi, Oktoba 26, 2019, saa 8:00 mchana.

Ndege ya kwanza ya Boeing 787-8 Dreamliner iliundwa 2009, na hadi Septemba 2019, zimeshaundwa ndege za aina hiyo 894.


Ndege hiyo iliyopewa jina la Hifadhi ya Kisiwa cha Rubondo (Rubondo Island) itapokelewa na wananchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

 

Hii inakuwa ndege ya 8 kati ya ndege 11 zilizonunuliwa na Serikali kwa lengo la kuimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kukuza utalii na uchumi.

Comments are closed.