The House of Favourite Newspapers

JPM Mgeni Rasmi Mkutano wa 33 wa Kitaifa wa ALAT

0
Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa ALAT, Stephen Mhapa, Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Gulamhafeez Mukadamu na Kaimu Katibu Mkuu, Abdallah Ngodu.

 

JUMUIYA ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) inatarajiwa kufanya mkutano wake wa 33 kitaifa katika Jiji la Mbeya Agosti 19 mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Gulamhafeez Mukadamu wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar.

“Katika mkutano huo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli huku wajumbe kutoka halmashauri zaidi ya 163 nchini wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo,” alisema Mukadamu.

 

Makamu Mwenyekiti wa ALAT, Stephen Mhapa akizungumza na wanahabari.

 

Aidha kunatarajiwa kuwa na ugeni wa kimataifa kutoka nchi za Kenya, Rwanda, Uganda na Burundi ambapo mkutano huo unalenga hasa kutoa fursa kwa wafanyabiashara, sekta binafsi na taasisi zisizo za serikali kutangaza biashara na kuonyesha ubunifu katika bidhaa na huduma zao.

 

NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

=====

LIVE: Rais Magufuli, Pierre Nkurunzinza Wawahutubia Wananchi Ngara – Kagera

Leave A Reply