The House of Favourite Newspapers

Jubilee Yawakumbuka Wazee, Watoto Kupata Bima za Afya Kiurahisi

0
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Afya ya Jubilee, Dk Harold Adamson, akizungumza na wadau (hawapo pichani) kwenye uzinduzi huo. 

Dar es Salaam, 21 Januari 2023: Kampuni ya Bima ya Afya ya Jubilee imewakumbuka wazee na watoto kwa kuwatengenezea vifurushi maalum vitakavyowahakikishia kupata huduma za afya.

Vifurushi hivyo vinavyoitwa J Care Senior (kwa wazee kuanzia miaka 61) na J Care Junior (kwa watoto wenye miaka sifuri hadi 17) vinatarajiwa kusaidia sera ya serikali ya kutoa bima ya afya kwa wote.

 

wadau wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya bima ya afya ya Jubilee, Dk Harold Adamson, amesema huduma hizo mbili zimeanzishwa ili kukidhi mahitaji ili kutunza makundi hayo maalum.

Hivyo basi Tunajivunia na kusema kuwa sisi ni kampuni ya bima ya afya ya kwanza katika sekta binafsi kuwa na bidhaa hizi sokoni. Ni bidhaa ambazo zimekuja kutatua tatizo la watanzania wengi ambao walikuwa wana uhitaji mkubwa kwenye jamii yetu.

“Tuna imani kwamba huduma hizi zinaenda kutatua changamoto kadhaa katika jamii yetu kwenye sekta ya bima ya afya. Pia kupitia huduma hizi mpya kwa haya makundi maalumu ambayo yamesaulika kwa muda mrefu, sasa tunaunga mkono jitihada za serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika ajenda muhimu ya bima ya afya kwa wote,” alisema.

Wadau katika picha ya pamoja baada ya hafla hiyo.

Mkurugenzi huyo alisema Jubilee ndiyo kampuni ya kwanza binafsi kuwa na huduma maalum kwa wazee na watoto.

Huduma ya J Care Senior inatarajiwa kuwasaidia wazee kupata huduma mbalimbali kama vile uchunguzi wa kiafya kwa ajili ya mwili wote, usimamizi wa mtindo wa maisha, klabu ya afya kwa wazee na manufaa mengine.

Kwa upande mwingine, huduma ya J Care Junior ni mahsusi kwa ajili ya watoto kuanzia miaka 0 hadi 17. Huduma hii ni ya mtoto pekee na inakuja na manufaa mengine kama vile tohara, magonjwa ambayo mtoto amezaliwa nayo kama vile tundu kwenye moyo, sickle cell na kadhalika.

Serikali ipo katika mchakato wa kutunga sheria itakayo sukuma watu wote kuwa na bima ya afya, ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu bora.

Muswada wa sheria hiyo unatarajiwa kupelekwa bungeni mwisho wa mwezi huu na serikali inatarajia huduma hiyo itaanza mwezi Julai mwaka huu.

Leave A Reply